MAREKANI-SYRIA-URUSI-IRAN-USHIRIKIANO

Obama: "Washington iko tayari kushirikiana na Moscow na Tehran kuhusu Syria"

Rais wa Marekani Barack Obama katika jukwaa la Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 28, 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama katika jukwaa la Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 28, 2015. AFP/AFP

Rais wa Marekani Barack Obama amesema Jumatatu wiki hii mbele ya wajumbe wa Umoja wa Mataifa kuwa yuko tayari kushirikiana na Urusi na Iran, ili kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro wa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Urusi na Iran ni washirika wa karibu wa Rais wa Syria Bashar Al Assad.

Lakini ameshutumu msaada unaopewa Bashar al-Assad, ambaye Moscow na Tehran wanataka abaki madarakani.

Katika hotuba yake mbele ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Marekani pia amesema Marekani " haitaki kurudi kwa vita baridi " na Urusi licha ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Moscow kwa kuingilia kijeshi Ukraine.

Rais Obama ametetea mpango wa nyuklia uliosainiwa mwezi Julai na Iran na kutoa wito kwa Bunge la Marekanikuiondolea vikwazo vya kiuchuminchi ya Cuba " ambayo haipaswi kuwa katika nafasi hiyo."

" Marekani iko tayari kushirikiano na nchi zote, ikiwa ni pamoja na Urusi na Iran kwa kutatua mgogoro unaoendelea kushuhudiwa nchini Syria ", amesema Obama.

" Lakini tunapaswa kutambua kwamba baada ya mauaji mengi, hakuna kurudi kwa hali kama ilivyo kabla ya vita ", Rais Barack Obama ameongeza.

Marais wa Urusi Vladimir Putin na Iran Hassan Rouhani wanatazamia kuzungumza Jumatatu wiki hii katika jukwaa ya Umoja wa Mataifa.

Obama smetuhumiwa Assad wa kuwa " mjeuri ", " ambaye  amekua akiwaua watoto wasio na hatia ". Amewaomba marais wa Iran na Urusi kutoendelea kumuunga mkono Bashar Al Assad, akionya kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi

Urusi na Iran wanasema kwamba kipaumbele kwa sasa ni kupambana dhidi ya wanamgambo wa kundi la Islamic State, ambalo linadhibiti nusu ya nchi ya Syria, wala si mabadiliko ya utawala wa Damascus. Putin anatazamia kuupendekeza Umoja wa Mataifa kuunda muungano mpana wa kupambana dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State (IS).