MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

California: watuhumiwa wawili watambuliwa na wameuawa

Maafisa wa polisi wakiwasaka watuhumiwa wa mauaji katika Kaunti ya San Bernardino Desemba 2, 2015.
Maafisa wa polisi wakiwasaka watuhumiwa wa mauaji katika Kaunti ya San Bernardino Desemba 2, 2015. AFP/AFP

Wahusika wawili wa mauaji mabaya kutokea nchini Marekani kwa muda wa miaka mitatu, ambayo yaligharimu maisha ya watu 14 Jumatano hii katika kaunti ya San Bernardino, ni mwanaume na mwanamke wenye umri wa miaka 28 na 27, lakini wameuawa, kwa mujibu wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

Mwanaume anaitwa Syed Farook, raia wa Marekani, mwenye umri wa miaka 28, mfanyakazi wa mji huo wa California, na alikuwa akiambatana na mwanamke mwenye umri wa miaka 27, Tashfeen Malik, ambaye uraia wake haujulikana bado, mkuu wa polisi ya kaunti ya San Bernadino, Jarrod Burguan, amesema.

Shambulizi hilo lilitokea Jumatano saa 2:30 usiku saa za Afrika ya Kati (sawa na saa 5:30 saa za California), na kusababisha vifo vya watu14 na kuwajeruhi wengine 17, kwa mujibu wa polisi katika mji huo.

Majengo ambapo tukio hilo limetokea kunapatikana kituo kinachohudumia watoto wenye ulemavu, Idara mablimbali za manispaa na makampuni. Watuhumiwa wawili wameiuawa na mmoja amekamatwa, mkuu wa polisi katika mji huo amehakikisha, saa tano baada ya mauaji hayo.

Barack Obama Jumatano alituma rambirambi zake kwa familia za wahanga wa mauaji hayo, huku akilaumu matukio yanayotokea mara kwa mara nchini Marekani. "Kuna hatua ambazo tunaweza kuchukua, si kutokomeza mauaji hayo, lakini kuboresha hali ya Usalama mashambulizi kama hayo yasitokei tena kwa hali kama hii", rais wa Marekani amesema kwenye runinga ya CBS.