Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Shule zote za Los Angeles zafungwa

Basi la shule katika mji wa Los Angeles (California), Oktoba 8, 2008.
Basi la shule katika mji wa Los Angeles (California), Oktoba 8, 2008. AFP/Getty/AFP/
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Shule zote za umma za Los Angeles zimefungwa Jumanne hii baada ya tishio ambalo limetajwa kuwa la kweli na kulenga maeneo kadhaa. Hatua ambayo iliwakabili zaidi ya wanafunzi nusu milioni na inakuja katika mazingira ya mashambulizi ya hivi karibuni jijini Paris na San Bernardino.

Matangazo ya kibiashara

Vitisho pia vimelenga Shule zote mjini New York Jumanne hii, lakini polisi imevitaja vitisho hivyo kwamba "si vya kweli", polisi imesema baada ya muda kidogo asubuhi.

Uamzi wa kufungwa kwa shule za Los Angeles umetangazwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa visomo, saa 1:30 asubuhi saa za Losa Angeles (sawa na 9:30 saa za kimataifa). Hatua hii inahusu zaidi ya wanafunzi 640,000 wa shule mbalimbali ikiwa ni pamoja na shule za chekechea, za msingi na za sekondari za umma katika taasisi zaidi ya 1,000.

Ilikua "tishio la kweli", mkaguzi wa elimu katika mji wa Los Angeles amesema kwenye akaunti yake ya Twitter.

Ukaguzi wa elimu katika mji wa Los Angeles ulipewa taarifa mapema alfajiri na polisi kuhusu vitisho hivyo, ambapo polisi ilitaja kuwa huenda baadhi ya vilipuzi vilikua vimewekwa katika "mifuko midogo inayobebwa mgongoni na katika vifaa vingine", mkurugenzi wa shule za umma za Los Angeles, Ramon Cortines, amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi.

Polisi "imepokea mapema leo asubuhi tishio la kielektroniki ambalo lilikua linahusu usalama wa shule zetu", amesema Steve Zipperman, mkuu wa polisi wa Los Angeles anayehusika na usalama wa shule, wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.