Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Safari za ndege kati ya Marekani na Cuba kuanza

Ubalozi wa Marekani mjini Havana (Cuba) ambapo bendera za Cuba zinapepea, Julai 27, 2015.
Ubalozi wa Marekani mjini Havana (Cuba) ambapo bendera za Cuba zinapepea, Julai 27, 2015. Reuters/ Alexandrte Meneghini
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Marekani na Cuba zimefikia mwafaka wa kuanzisha tena safari za ndege kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, haijafahamika ni lini safari hizo zitaanza kwa sababu mazungumzo bado yanaeendelea.

Hatua hii inakuja mwaka mmoja sasa tangu nchi hizo mbili zilipoweka kando tofauti zao na kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia.

Kwa sasa abiria wanaokwenda katika nchi hizo mbili wanalazimika kutokea katika nchi nyingine.

Mwezi Disemba Cuba na Marekani walitangaza kuwa walikubaliana kuboresha uhusiano wao baada ya zaidi ya miaka 5.

Mwakilishi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ndiye aliyefanya jitihada za kukutanisha viongozi wa mataifa hayo mawili kwa lengo la kufufua uhusiano kati ya Havana na Washington.

Ilikuwa ni moja ya matukio ya mwisho ya vita baridi. Marekani na Cuba zilianza kuwa maadui tangu kuvunjika kwa mahusiano ya kidiplomasia mwezi Januari mwaka 1961, baada ya rais wa Marekani Dwight Eisenhower kuchukua uamzi.

Tangu ukuta wa Berlin kuanguka, rais Barack Obama alikubali kushindwa kwa sera za Marekani kwa Havana, na nchini Cuba , Raul Castro, aliyemrithi ndugu yake Fidel Castro, alianzisha hatua za ufunguzi wa sekta ya kiuchumi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.