MAREKANI-SIASA-SILAHA

USA: Obama mbioni kuchukua hatua dhidi ya umiliki wa silaha

Rais wa Marekani Barack Obama akizungukwa na binti zake Malia (kushoto) na Sasha (wa pili kutoka kulia), pamoja na mke wake Michelle Obama (kulia), Januari 3, 2016, Washington.
Rais wa Marekani Barack Obama akizungukwa na binti zake Malia (kushoto) na Sasha (wa pili kutoka kulia), pamoja na mke wake Michelle Obama (kulia), Januari 3, 2016, Washington. AFP/AFP

Akitokea Hawaii, rais wa Marekani Barack Obama ameanza kujibu juu ya udhibiti wa silaha za moto na mipango inayotarajiwa wiki hii, ambayo inapaswa hata hivyo kukabiliwa na mipaka ya madaraka yake.

Matangazo ya kibiashara

Bila msaada wa Baraza la Wawakilishi, Barack Obama anaweza kuchukua hatua anazoruhusiwa na katiba ambazo zinakabiliwa na mipaka ya madaraka yake.

Mwanzoni mwa mwaka wake wa mwisho katika Ikulu ya White House, Rais wa Marekani anataka kuonyesha hisia baada ya miaka saba akiwa madarakani, ambapo visa vya mauaji kwa kutumia silaha za moto vilishuhudiwa kwa wingi nchini Marekani. Obama amekua akielezea masikitiko yake kufuatia visa hivyo.

Bila kujali Baraza la Wawakilishi na kulingana na sheria za kirais, Obama anajua kuwa anaweza kuwa chini ya hatua za kisheria, na hivyo hali hiyo ikawekwa katika mjadala wakati wa kampeni za urais.

"Hivi karibuni hatutokua na uwezo wa kumiliki tena silaha", bilionea Donald Trump amesema Jumatatu hii, kwa kauli ya kebehi. Donald Trump anawania katika kinyan'ganiro cha urais katika kambi ya chama cha Republican.

Obama anatazamiwa kukutana Jumatatu hii mchana na Waziri wa sheria Loretta Lynch kuchunguza mfumo unaowezekana. Matangazo yatafuata haraka. Alhamisi usiku, Obama atajibu maswali ya raia moja kwa moja kwenye CNN.