Afghanistan: mwanajeshi wa Marekani auawa

Askari polisi wa Afghanistan akipiga kambi katika mji wa Marjah kusini mwa Afghanistan, Desemba 23, 2015.
Askari polisi wa Afghanistan akipiga kambi katika mji wa Marjah kusini mwa Afghanistan, Desemba 23, 2015. AFP/AFP/

Operesheni ya vikosi maalum katika mji wa Marjah katika mkoa wa kusini wa Helmand, kusini mwa Afghanistan, imesababisha hasara kubwa kwa majeshi ya Marekani na Afghanistan, afisa wizara ya ulinzi ya Marekani ametangaza Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

"Najua kwamba kuna wanajeshi waliojeruhiwa kwa pande zote mbili, Marekani na Afghanistan", chanzo hiki ambacho hakikutaka kitajwe jina kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, bila kutoa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa kituo cha NBC News, mwanajeshi wa Marekani ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika operesheni hiyo.

Helikopta ya kijeshi ambayo imekua ikitua kwa kuwasafirisha wanajeshi waliojeruhiwa imedondoka baada ya mlipuko wa bomu uliotokea karibu na eneo ambapo helikopta hiyo ilikua ikijaribu kutua.

Kanali Michael Lawhorn, msemaji wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi NATO nchini Afghanistan amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba helikopta hiyo ya jeshi la Marekani ilikuwa na "matatizo ya kiufundi" lakini ameongeza kuwa "haikudondoshwa kwa bomu."