MAREKANI-USALAMA

Barack Obama: "udhibiti wa bunduki wapaswa kukomeshwa Marekani"

Barack Obama akisononeshwa na udhibiti wa silaha Marekani.
Barack Obama akisononeshwa na udhibiti wa silaha Marekani. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Barrack Obama amezindua sera mpya ya kununua na kumiliki silaha nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akioneakana mwenye huzuni na kulemewa na hisia na hata kutoa machozi, rais Obama amesema akiwakumbuka watu waliuawa kwa kushambuliwa anajisikia vibaya sana.

Mpango huu mpya unalenga kuwachunguza zaidi, wale wanaotaka kununua silaha na pia wauzaji kutafuta leseni maalum na njia za Kieletriniki kutumiwa kuchunguza silaha zinazouzwa.

Obama ameidhinisha mpango huu bila ya idhini ya Bunge la Congress, uamuzi ambao unapingwa na wabunge wa upinzani wa Republican.

Obama amesisitiza kuwa ni lazima hatua zichukuliwe.