MAREKANI-WIZI

Marekani: mtu akamatwa kwa kujaribu kumuiba mbwa wa Obama

Mbwa wawaili wa familia ya Obama, Bo (kushoto) na Sunny (dkulia), Agosti 19, 2013, Washington.
Mbwa wawaili wa familia ya Obama, Bo (kushoto) na Sunny (dkulia), Agosti 19, 2013, Washington. AFP/Maison Blanche/AFP/

Mtu ambaye anaonekana alipanga kumuiba mmoja wa mbwa wa familia ya Obama katika Ikulu ya Marekani alikamatwa wiki hii mjini Washington, vyombo vya habari vya Marekani vimearifu Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Scott Stockert, mwenye umri wamiaka 49, raia wa North Dakota (Kaskazini mwa Marekani), alikamatwa Jumatano na Idara ya Ulinzi wa rais wa Marekani katika hoteli moja katika mji mkuu wa Marekani, Washington, kwa mujibu wa kituo cha NBC, baada ya tahadhari ya miundo ya mtu kutoka ofisi ya Idara ya Minnesota.

Kwa mujibu wa Idara ya Ulinzi wa rais wa Marekani, mtu huyo alitaka kumuiba mbwa anayejulikana kwa jina la Bo, moja ya mbwa mbili wa zamani wa familia ya Obama kutoka Ureno. Mbwa mwengine ni wa kike aitwaye Sunny.

Mtu huyo aliwaambia polisi kuwa ni mtoto wa John F. Kennedy na Marilyn Monroe na anaitwa Yesu Kristo. Lakini alikuwa na bunduki mbili katika gari lake, risasi zaidi ya 300, panga pamoja na rungu. Jambao ambalo lilipelekea anakabiliwa na mashataka ya kumiliki silaha isiyosajiliwa kwa vyombo husika.

Scott Stockert alionekana Alhamisi mbele ya mahakama mjini Washington. Jaji alimuachilia huru kwa dhamana Ijumaa wiki hii, akitakiwa kukaa mbali na Ikulu ya Marekani na Makao Makuu.