MEXICO-AJALI

Mexico: watu 21 wafariki katika ajali ya basi

Basi lililokuwa limebeba wachezaji limeanguka mtoni na kusababisha vifo vya watu 21 Mexico, Januari 10, 2016.
Basi lililokuwa limebeba wachezaji limeanguka mtoni na kusababisha vifo vya watu 21 Mexico, Januari 10, 2016. AFP/AFP/

Basi lililokuwa limebeba wachezaji wa mpira na mashabiki wao imegonga daraja na kuanguka mtoni Jumapili hii nchini Mexico. Ajali hii imesababisha vifo vya watu 21, maafisa wa usalama nchini Mexico wamebaini.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengine thelathini wamejeruhiwa katika ajali hiyo, ambayo ilitokea katika mji wa Atoyac katika jmbo la Veracruz (mashariki), karibu na Ghuba ya Mexico.

Uchunguzi wa awali umepelekea kutahmini kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni mwendo wa kasi, ambapo dereva alipoteza udhibiti wa gari na kugonga kizuizi cha daraja, kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Jimbo hilo.

Awali idadi ya waliofariki iliyotolewa na serikali ilikuwa ya watu 16, lakini miili mingine imegundua katika basi, ambalo limeharibika vibaya.

Basi hilo lilikua likiwabeba wachezaji waliokua njiani kuelekea kushiriki mchuano, kwa mujibu wa maafisa wa serikali, na watoto kadhaa walikuwa katika gari hilo.