HAITI-TETEMEKO-KUMBUKUMBU

Haiti yatoa heshima kwa wahanga miaka sita baada ya tetemeko

Rais wa haiti Michel Martelly (wa 2 kulia) na Waziri Mkuu Paul Evans (wa 2 kushoto) wakiweka shada za maua wakati wa sherehe ya kumbukumbu, Januari 12, 2016 katika mji wa Port-au-Prince kwa kuwakumbuka wahanga wa tetemeko la Januari 12, 2010.
Rais wa haiti Michel Martelly (wa 2 kulia) na Waziri Mkuu Paul Evans (wa 2 kushoto) wakiweka shada za maua wakati wa sherehe ya kumbukumbu, Januari 12, 2016 katika mji wa Port-au-Prince kwa kuwakumbuka wahanga wa tetemeko la Januari 12, 2010. AFP/AFPL

Jumanne hii, Haiti imetoa heshima ya kumbukumbu kwa watu zaidi ya 200,000 waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi, miaka sita iliyopita. Tetemeko hilo la ardhi lililikumba eneo la mji mkuu wa Port-au-Prince na kusini-mashariki.

Matangazo ya kibiashara

"Tumekuja kutoa heshima kwa wale tuliowapotea, lakini hasa kwa kuzingatia kuwa tunahusika kwa kile kilichotokea kwa sababu, hatukua tulijianda vizuri", Rais Michel Martelly amesema baada maadhimisho rasmi.

"Watu hawakuwa katika usalama ili kuepuka janga hili", Rais Michel Martelly ameongeza.

Mapema Jumanne hii asubuhi, Rais wa Haiti na Waziri Mkuu Paul Evans wameweka shada la maua kwenye kaburi la kumbukumbu, liliyoko kaskazini mwa mji mkuu, ambapo walizikwa maelfu ya wahanga katika makaburi la pamoja.

Bendera imepanishwa nusu mlingoti nchini kote. Raia wa Haiti wamealikwa na mamlaka kwa kutafakari ili "kuimarisha upendo, mshikamano na kusaidizana kama ilivyokua wakati janga hilo lilipotokea", Tangazo la serikali limebaini.

Januari 12, 2010,kabla ya 11:00 jioni, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7 kwa kiwango cha Richter lilisababisha uharibifu wa majengo zaidi ya 300,000, na kuua watu zaidi ya 200,000 na kusababisha watu milioni na nusu kubaki bila makazi.