VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Venezuela: mgogoro wa taasisi wadhoofisha shughuli za Bunge

Picha ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro (kushoto) tarehe 12 Novemba 2015 na picha ya spika wa Bunge, Henry Ramos Allup ya Desemba 8, 2015.
Picha ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro (kushoto) tarehe 12 Novemba 2015 na picha ya spika wa Bunge, Henry Ramos Allup ya Desemba 8, 2015. AFP/AFP

Mgogoro wa kitaasisi unaoikumba Venezuela tangu upinzani kutawala Bunge umezorotesha shughuli za taasisi hiyo Jumanne hii. Bunge limeahirisha shughuli zake baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu Jumatatu wiki hii wa kubatilisha hatua yoyote ya Bunge.

Matangazo ya kibiashara

Akitoa mfano wa idadi isiyotosha ya Wabunge, Spika wa Bunge, anayepinga sera ya Hugo Chavez, Henry Ramos Allup, amesimamisha shughuli za Bunge hadi Jumatano hii, waandishi wa habari wa shirka la habari la Ufaransa AFP wameshuhudia Jumanne hii.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Bunge, upinzani umekua ukiendesha Jumanne hii mashauriano na wanasheria wake ili kukabiliana na uamuzi wa Mahakama Kuu (TSJ), ambayo upinzani unaona kuwa inatumikia kwa sera za hayati rais Hugo Chavez (madarakani tangu mwaka 1999 hadi 2013).

Upinzani umetangaza kuwa unapanga "kuzungumzia kuhusu undani" wa uamuzi wa Mahakama kuu (TSJ) Jumatano hii wakati Bunge litaerejelea shughuli zake.

Baadaye Jumanne hii, Henry Ramos Allup amebaini kuwa alikuwa na mawasiliano kadhaa na utawala wa Chavez. Amebaini kwamba Makamu wa rais wa Venezuela, Aristobulo Isturiz, ambaye alikuwa aliongea naye kwenye simu, anaweza "kuwa msuluhishi katika mawasiliano kati ya serikali na upinzani."

Katika mgogoro huo wa kitaasisi, Bunge la Venezuela, awali lilipunguza kasi katika mvutano na serikali inayotembelea kwenye sera za hayati rais Hugo Chavez, na kubaini kwamba kikao chake kinapaswa kufanyikaJumanne hii, licha ya uamuzi wa TSJ siku moja kabla wa kubatilisha hatua yoyote ya bunge.

Jumatatu, mvutano uliojitiokeza kati ya pande hizo mbili ulichukua mwelekeo mpya baada ya tangazo la TSJ, ambayo inaona kama "batili" vitendo vya Bunge liliopita na lijalo, kama wabunge watatu wa upinzani walioapishwa wiki iliyopita licha ya kusimamishwa kwao watasalia kwenye nafasi zao.