FIFA-UFISADI

FIFA: Alfredo Hawit akubali kusafirishwa Marekani

Alfredo Hawit wakati huo rais wa mpito wa CONCACAF na Shirikisho la la Soka la Honduras, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 5, 2015, Tegucigalpa.
Alfredo Hawit wakati huo rais wa mpito wa CONCACAF na Shirikisho la la Soka la Honduras, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 5, 2015, Tegucigalpa. AFP

Mmoja wa makamu rais wa FIFA, Alfredo Hawit kutoka Hunduras, aliokamatwa mjini Zurich mapema mwezi Desemba na kusimamishwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, amekubali Jumatano hii kusafirishwa nchini Marekani, Mahakama ya Bern imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Hawit mwenye umri wa miaka 64, pia rais wa shirikisho la Soka la Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF), aliwekwa kizuizini katika lengo la kusafirishwa Desemba 3, 2015, kwa ombi la mamlaka ya Marekani.

Alikua alisimamishwa kwenye wadhifa wake na FIFA siku moja baadaye.

Vyombo vya Marekani vinamtuhumu kuwa alipokea rushwa ya mamilioni kadhaa ya doal kwa ajili ya kuyapa makampuni Haki ya soko linalohusiana na usambazaji wa mashindano katika Amerika ya Kusini.

Katika mahojiano yake ya kwanza na polisi ya mjini Zürich, baada ya kukamatwa kwake, Alfredo Hawit alipinga kusafrishwa nchini Marekani.

Jumatano, katika mahojiano ya pili, raia huyo wa Honduras hatimaye amekubali kusafirishwa nchini Marekani.

Kulingana na sheria kuhusu kusaidizana kimataifa dhidi ya uhalifu, polisi ya Marekani ina muda wa siku kumi ili kumgharamia chakula na kumsafirisha nchini Marekani.