MAREKANI-AJALI

Marekani: helikopta mbili za kijeshi zatoweka

Walinzi wa pwani wa Marekani, 7 Machi 2013.
Walinzi wa pwani wa Marekani, 7 Machi 2013. AFP/GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/Archives

Walinzi wa pwani nchini Marekani wamekua wakitafuta Ijumaa hii helikopta mbili za kijeshi ziliokua zikibeba wanamaji kumi na mbili karibu na pwani ya kisiwa cha Oahu, katika visiwa vya Hawaii, baada ya jeshi kutoa tahadhari kuwa helikopta hizo zimegongana, msemaji wa maafisa wa waokowaji ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Matangazo ya kibiashara

"Tumepata eneo kunakoonekana mabaki ya helikopta hizo, kilomita nne kutoka pwani na tumeanzisha zoezi la kutafuta katika eneo hilo. hatujapata mtu yeyote mpaka sasa", msemaji wa maafisa wa waokoaji amebaini, akiongeza kwamba wamepokea simu muda mfupi kabla ya usiku wa manane Alhamisi hii (sawa na saa 3:38 saa za kimataifa).

"Walinzi wa pwani wameingilia kati baada ya kuelezwa kwamba helikopta mbili za kijeshi zimegongana katika pwani ya kaskazini mwa Oahu katika bahari ya Pasifiki", ameeleza msemaji. "Taarifa ambazo tumepokea kutoka mabaharia ni kwamba helikopta mbili kati ya helikopta zao ziliokua zikiendesha shughuli karibu na kisiwa hiki pamoja na wafanyakazi sita kwa kila helikpota zimetoweka."

Kwa mujibu wa kikosi cha majini, helikopta mbili zinazotafutwa ni helikopta kubwa za uchukuzi aina ya CH-53.Zilikua zikiendesha harakazi mbalimbali katika visiwa vya Hawaii, kwa kusaidia ujumbe wa kikosi cha majini kwa kusafirisha askari katika uwanja wa mapambano, vifaa vya kivita vya kijeshi, usiku na mchana katika hali zote za mazingira.