MAREKANI-IRAN-WAFUNGWA

Wamarekani 4 wenye asili ya Iran wasafirishwa Uswisi

Mwandishi wa habari wa Washington Post, raia wa Iran mwenye asili ya Marekani Jason Rezaian Septemba 10, 2013 mjini Tehran.
Mwandishi wa habari wa Washington Post, raia wa Iran mwenye asili ya Marekani Jason Rezaian Septemba 10, 2013 mjini Tehran. AFP/AFP/

Wafungwa wane raia wa Marekani wenye asili ya Iran walioachiwa huru Jumamosi nchini Iran wamesafirishwa Jumapili hii na "ndege maalum ya Uswisi" katika mji wa Bern nchini Uswisi, runinga ya serikali ya Iran imearifu.

Matangazo ya kibiashara

Mwaandishi wa habari wa gazeti la Washington Post, Jason Rezaian, Mchungaji Saeed Abedini, aliyekuwa baharia Amir Hekmati Khosravi na mtu wa nne aitwaye Nosratollah Khosravi waliachiwa huru Jumamosi katika mfumo wa kipekee wa operesheni na Marekani ya kubadilishana wafungwa. Marekani iko mbioni kuwaachia huru wafungwa saba wa Iran.

Runinga ya serikali ya Iran imeongeza kuwa wafungwa saba wa Iran wanaozuiliwa nchini Marekani wanaweza "kuachiwa huru (Jumapili hii)."

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Gholam-Ali Koshroo amesema kuwa Uswisi, ambayo inawakilisha maslahi ya Marekani nchini Iran imefanya "kazi kubwa tena muhimu" kwa operesheni ya kipekee ya kubadilishana wafungwa kati ya nchi hizi mbili ambazo hazikua na uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1980.

Operesheni ya kubadilishana wafungwa inafanyika siku ya kihistoria ya makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu yalipotekelezwa.

Raia hawa saba wa Iran watakaoachiwa huru na Marekani, ikiwa ni pamoja na sita ambao wana uraia wa mataifa mawili, walikua wakishitakiwa au tayari wamesha hukumiwa kwa kosa la kuiuza Iran vifaa vya viwanda kwa ukiukaji wa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran.