MAREKANI-IRAQ-UTEKAJI NYARA

Washington yawatafuta Wamarekani watatu waliotekwa nyara Iraq

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby, Januari 6, 2015 Washington.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby, Januari 6, 2015 Washington. AFP/AFP/

Mamlaka za Marekani na Iran zinawatafuta tangu Jumapili mwishoni mwa juma hili Wamarekani watatu waliotekwa nyara nchini Iraq, chanzo cha polisi ya Iraq na Wizara ya Mambo ya nje vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi mwenye cheo cha kanali nchini Iraq ambaye hakutaka jina lake litajwe amethibitisha kwamba Wamarekani watatu na mkalimani wao, raia wa Iraq wametekwa nyara kusini mwa mji wa Baghdad, na vikosi vya Iraq vimeanzisha oparesheni kuhakikisha wamepatikana.

Watekaji nyara wanasadikiwa kuwa wanamgambo, ambao walikua wamevaa sare za kijeshi, afisa huyo wa polisi amesema. Kuhusu Wamarekani, ameongeza: "Hatujui kazi waliokuwa wakifanya".

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, John Kirby, amesema mapema kwa ufupi katika barua pepe kuwa "Wamarekani wametoweka nchini Iraq ", lakini bila kutaja idadi yao au mahali ambapo walitowekea.

Hakusema pia kama walikuwa askari au makandarasi wa ujenzi wa ubalozi mkubwa wa Marekani mjini Baghdad.

"Tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mamlaka ya Iraq kwa kuwatafuta na kuwapata watu hawa", amesema afisa huyo wa Marekani.

John Kirby ameeleza yale Washington inayosisitiza kila mara kwamba raia wake wanaathirika au wako katika hatari kila mahali: "Ulinzi na usalama wa raia wa Marekani ni kipaumbele chetu cha juu".

Marekani ilijiondoa kijeshi nchini Iraq mwezi Desemba 2011, lakini walijihusisha tena upya, kwa kiwango cha askari kadhaa wasio wapiganaji, tangu majira ya joto mwaka 2014 kwa kusaidi mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State.