Marekani: shughuli za kusafisha miji zaendelea
Shughuli za kusafisha maeneo mbalimbali Jumapili hii katika pwani ya Mashariki mwa Marekani, iliyokumbwa Ijumaa na Jumamosi na kimbunga cha theluji kiliyosababidha vifo vya watu 18 na kuzorotesha shughuli mbalimbali katika miji mikubwa, ikiwa ni pamoja na mji wa New York, imeendelea Jumapili hii.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kimbunga hiki kinachojulikana kwa jina la Jonas kilisababisha kiwango kikubwa cha theluji kudondoka na kuendelea kwa zaidi ya masaa 36 hadi usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.
Katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Virginia, theluji zimeanguka hadi kwenye kiwango cha mita moja.
Katika mji wa New York, rekodi imepiga katika eneo la Central Park, kwa sentimita 67 kwa siku nzima.
Rekodi imepiga pia katika mji wa Washington, ambapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles ulikua chini ya sentimeta 56 za unga wa theluji ndani ya masaa 24.
“Tuko katika kipindi cha matukio ya hali mbaya ya hewa”, amesema Meya wa mji wa New York, bill de Blasio, akibaini kwamba matukio ya hali hii yatakua ya kawaida.
Watu wasiopungua 18 wamepoteza maisha kutokana na mazingira ya hali hii ya hewa, kwa mujibu wa viongozi mbalimbali, Watu wa tano wamepoteza maisha katika jimbo la ew York, sita katika jimbo la North Caroline, watatu katika jimbo la Virgini, wawili katika mji wa Kentucky, mmoja katika mji wa Maryland na mwengine mmoja katika jimbo la Arkansas.
Katika jimbo la New Jersey, miji mingi ya pwani ya Kusini ya jimbo hilo imekumbwa na mafuriko pamoja a kukatika kwa umeme.
Katika jimbo la North Caroline, watu 51,000 walikua hawana umeme Jumapili hii asubuhi.
Ukubwa wa tukio hili umesababisha mamlaka ya mji wa Washington na Baltimore kusitisha usafiri wa umma mwishoni mwa juma hili.
Viwanja vya ndege pia vimekumbwa na hali hii. Safari 11,000 za ndege kwa mchana wa siku tatu wa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili zimefutwa kwa mujibu wa tovuti ya FlightAware.