MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Siku muhimu kwa kura za mchujo Marekani

Wapiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Arlington, Virginia tarehe 1 Machi mwaka 2016.
Wapiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Arlington, Virginia tarehe 1 Machi mwaka 2016. REUTERS/Gary Cameron

Mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton anaelekea kujenga nafasi itakayomuwezesha kushinda katika kile kinachojulikana kama Jumanne Kuu.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni siku muhimu ya kura za mchujo, wakati chama cha Republican kinajaribu kuzuia mbio za mgombea wake anayeongoza Donald Trump.

Ikiwa zimebakia saa chache , Clinton na Trump wameonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kupata wajumbe wengi kuwapigia kura kwenye majimbo 11 katika kura za mchujo kwa kila chama.

Trump amekosolewa vikali Jumatatu hii baada ya kushindwa katika mahojiano kulishutumu kundi la kibaguzi la Ku Klux Klan na kiongozi wake wa zamani David Duke, ambaye amesema anamuunga mkono Trump.