MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Trump na Clinton wawashinda washindani wao "Jumanne Kuu"

Hillary Clinton na Donald Trump waonekana kuwa washindi katika vyama vya Democratic na Republican katika majimbo kadhaa ya kura za mchujo za "Jumanne Kuu" kupigwa.
Hillary Clinton na Donald Trump waonekana kuwa washindi katika vyama vya Democratic na Republican katika majimbo kadhaa ya kura za mchujo za "Jumanne Kuu" kupigwa. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files

Matokeo ya kwanza ya mchujo wa "Jumanne Kuu" yametangazwa katika majimbo sita kati ya 11. Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic na Donald Trump kutoka chama cha Republican wanaongoza, kulingana na makadirio ya vyombo vya habari vya Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Democratic

Kwa sasa, kulingana na utabiri wa hivi karibuni, Hillary Clinton anasadikiwa kupata ushindi katika majimbo ya Alabama, Tennessee, Texas na Arkansas, ambapo mumewe Bill Clinton alikuwa mkuu wa jimbo. Waziri huyo wa zamani pia anaongoza katika majimbo ya Georgia na Virginia, majimbo mawili ya kusini mwa Marekani yenye watu wachache. Katika jimbo la Georgia, karibu 40% ya wapiga kura ni Wamerakni wenye asili ya Afrika, katika jimbo la Virginia ni 60%.

Kwa upande wake, Bernie Sanders ameshinda, kwa hakika, katika jimbo aliko zaliwa la Vermont, na anaongoza katika jimbo la Oklahoma. Anakabiliana na Hillary Clinton katika jimbo la Massachusetts.

Republican

Upande wa chama cha Republican, wagombea watano bado wanapambana. Kwa sasa, Donald Trump hajakabiliwa na dosari. Kulingana na tafiti, bilionea huyo amepata ushindi katika majimbo ya Tennessee, Massachusetts na Alabama. Ushindi ambao unaongezeka mafanikio aliopata mapema Jumanne jioni katika ,aji,bo ya Georgia, Virginia na Vermont.

Kwa sasa, majimbo pekee ambayo Donald Trumpatakua ameshindwa na mshindani mwenza kutoka chama cha Republican ni Oklahoma na Texas alikozaliwa Seneta Ted Cruz ambaye amepata ushindi mkubwa.

Lakini zaidi ya mafanikio, waangalizi wote wanaamini kwamba kushinda mara mbili kwa Ted Cruz inampelekea kubaki katika mbio hizi, lakini hajawa na ushawishi wa kuangusha au kubadili kura za Donald Trump ili aweze kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.