VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Bunge la Venezuela lakabiliwa na mzozo wa kitaasisi

Spika wa Bunge la Venezuela, Henry Ramos Allup mjini Caracas Machi 2, 2016.
Spika wa Bunge la Venezuela, Henry Ramos Allup mjini Caracas Machi 2, 2016. AFP

Bunge la Venezuela, lenye wabunge wengi kutoka kambi ya upinzani dhidi ya Rais Nicolas Maduro kutoka chama cha Kisochalisti, limemua Alhamisi hii kuomba upatanishi wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Amerika (OAS) katika mgogoro wa kitaasisi unaoendelea nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Bunge la Venezuela lenye wabunge wengi kutoka chama cha MUD tangu uchaguzi wa Desemba 6, limepitisha nakala inayoomba Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Amerika (OAS) "kuchunguza utekelezaji wa Ibara ya 20 ya sheria ihusuo demokrasia baina ya nchi za Amerika, kwa kuzingatia kwamba kumekuwa na uvunjaji wa Katiba unaovuruga demokrasia," pamoja na uamuzi utakaochukuliwa na Mahakama Kuu Jumanne wa kupunguza uwezo wa Bunge.

Mgogoro wa kitaasisi unaoikumba Venezuela tangu upinzani kutawala Bunge, wii mbili zilizopita, ulizorotesha shughuli za taasisi hiyo. Bunge liliahirisha shughuli zake baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kubatilisha hatua yoyote ya Bunge.

Katika mgogoro huo wa kitaasisi, Bunge la Venezuela, awali lilipunguza kasi katika mvutano na serikali inayotembelea kwenye sera za hayati Rais Hugo Chavez, na kubaini kwamba kikao chake kingelipaswa kufanyika Jumanne Februari 10, licha ya uamuzi wa TSJ siku moja kabla wa kubatilisha hatua yoyote ya bunge.

Jumatatu Februari 9, mvutano uliojitiokeza kati ya pande hizo mbili ulichukua mwelekeo mpya baada ya tangazo la TSJ, ambayo iliona kama "batili" vitendo vya Bunge liliopita na lijalo, kama wabunge watatu wa upinzani walioapishwa wiki kadhaa ziliyopita licha ya kusimamishwa kwao watasalia kwenye nafasi zao.