HONDURAS-MAUAJI-MAZINGIRA

Honduras: mwanaharakati wa mazingira Bertha Cáceres auawa

Wanaharakati wa Baraza la Mashirika ya kiraia ya Honduras akiwemo Bertha Caceres wakiandamana katika mji wa Tegucigalpa, Machi 31, 2011.
Wanaharakati wa Baraza la Mashirika ya kiraia ya Honduras akiwemo Bertha Caceres wakiandamana katika mji wa Tegucigalpa, Machi 31, 2011. AFP

Mwanaharakati wa mazingira kutoka Honduras, Berta Cáceres , ameuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi hii na watu wenye silaha wasiojulikana wakati ambapo alikua akirudi nyumbani kwake katika mji wa La Esperanza, kilomita 200 kaskazini magharibi ya Tegucigalpa, familia yake imesema.

Matangazo ya kibiashara

olisi imesema kuwa kiongozi wa Baraza la Mashirika kiraia ya Honduras (COPINH), ambaye aliwahi kutunukiwa tuzo kwa ajili ya utetezi wake wa mazingira, ameuawa na majambazi "lakini tunafahamu sote kwamba ni kutokana na ushupavu wake wa kupoambana dhidi ya uharibifu wa mazingira, hasa viumbe viishio katika sehemu mbalimbali za nchi hii," amesema mama yake, Berta Flores, kwenye runinga ya TV Globo.

"Polisi inasema ilikuwa ni katika lengo la kumuua lakini ni uhalifu wa kisiasa wa serikali ya Honduras," Carlos H. Reyes, kiongozi wa chama cha FNRP, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Kwa upande wa polisi, watu wasiojulikana wameingia ndani ya nyumba wakipitia mlango wa nyuma na walimuua kwa kumpia risasi nyingi, lakini sote tunajua kwamba ni uongo mtupu, wamemua kutokana na msimamo wake" kwa kupambana dhidi ya uharibifu wa mazingira, Carlos H.Reyes amesisitiza.

Bi Flores Ameongeza kuwa Tume ya Haki za Binadamu ya Amerika iliombakwa hatua za kumlindia usalama mwanaharakati Berta Caceres lakini jambo hilo halikufanyika, alikua akikabiliwa na vitisho kutoka kwa wale wanaotetea madini na makampuni ya kuzalisha umeme.

Berta Caceres alikuwa anajulikana kwa utetezi wake wa Mto wa Gualcarque, katika idara ya Santa Bárbara, Kaskazini-Magharibi mwa Honduras, ambapo kampuni moja inayopania kujenga bwawa la kuzalisha umeme, kampuni ambayo imetishia kuwanyima maji mamia ya wakazi wa eneo hilo.

Mama yake amesema Berta Cáceres hivi karibuni alitembelea eneo hilo" na alikabiliana kimaneno na askari na walinzi wa kampuni hiyo inayopania kujenga bwawa hilo. Na aliniambia kuwa kampuni hiyo inapaswa kuachana na mpango huo wa kujenga bwawa hilo la sivyo atakubali apoteze maisha ili raia wa eneo hilo wanufaike.