MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Romney na Cruz wamshambulia Donald Trump bila huruma

Mitt Romney wakati wa hotuba yake, Alhamisi MAchi 3, katika jimbo la Utah, MArekani.
Mitt Romney wakati wa hotuba yake, Alhamisi MAchi 3, katika jimbo la Utah, MArekani. REUTERS/Jim Urquhart

Aliyekuwa mgombea wa chama cha Republican kwa uchaguzi wa urais wa Marekani Mitt Romney, hii Alhamisi, Machi 3, amemshambulia kwa ukali Donald Trump. Amesema kwamba Donald Trump ni mchokozi mlafi na amejaa na chuki.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni mashambulizi makali dhidi Donald Trump.
Mitt Romney amesema kugombea kwa Donald Trump katika uchaguzi wa urais "kutapelekea" ushindi kwa Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic.

Donald Trump ni "tapeli", "mtu asiefaa," Romney amesema mara kadhaa katika mdahalo ulioandaliwa na kituo cha Fox News Alhamisi hii, Machi 3. "Ngoja niseme wazi, kama sisi Warepublican tutathubutu kumchagua mgombea Donald Trump, ushindi ambao tungeupata utakua umepelekwa na maji,"amesema Mitt Romney.

Bw Trump, anayeongoza kwenye kura za maoni kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz.

Seneta wa Texas Bw Cruz amesema Bw Trump ni sehemu ya mfumo fisadi wa Washington, uliofadhili kampeni ya Hillary Clinton mwaka 2008.

Bw Trump, anayeongoza kwenye kura za maoni kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Mitt Romney na Ted Cruz.

Bw Trump amempuuzilia mbali Romney na kumtaja kuwa “mgombea aliyefeli”. Amemtusi pia Ted Cruz kama “muongo”. Trump amesema Cruz hafai kuwa rais Marekani

Baadhi ya wanachama wakuu wa Republican wanasema Bw Trump hafai na kwamba hawezi kushinda urais dhidi ya chama cha Democratic.