MAREKANI-REAGAN

Mkee wa Rais wa zamani wa Marekani Nancy Reagan amefariki

Picha ya zamani ya Nancy Reagan, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, akisubiri kuwapokea wagombea wa chama cha Republican, Simi Valley, Septemba 7, 2011.
Picha ya zamani ya Nancy Reagan, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, akisubiri kuwapokea wagombea wa chama cha Republican, Simi Valley, Septemba 7, 2011. REUTERS/Chris Carlson/Pool/Files

Nancy Reagan, mke wa Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan, amefariki Jumapili hii, Machi 6 mjini Los Angeles kufuatia maradhi ya moyo. Nancy Reagan amefariki akiwa na umri wa miaka 94, Joanne Drake, msemaji wa Mkataba ya Reagan, amesema, akithibitisha taarifa iliotolewa na tovuti ya Marekani ya TMZ.

Matangazo ya kibiashara

Ronald Reagan, mumewe Nancy Reagan, alichaguliwa mwaka 1980 kuwa rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, na kisha alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne. Ronald Reagan alifariki mwezi Juni mwaka 2004. Mke wake, Nancy Reagan atazikwa upande wake katika eneo la Ronald Reagan Presidential Library katika mji wa Simi Valley, California (magharibi).

Historia ya mapenzi ya zaidi ya nusu karne

Mchezaji na muongozaji wa filamu zilizopendwa zaidi miaka hiyo ya nyuma, Nancy Davis, ambaye alikosolewa kwa ushawishi wake mkubwa kwa rais alipendwa kwa utetezi wake wa heshima na urithi wa kisiasa wa mtu ambaye alikuwa mumewe kwa miaka 52. Alionekana kwa msaada wake mkubwa kwa rais wa zamani (1981-1989) ambaye alifariki kwa ugonjwa wa Alzheimer. Ronald Reagan alifariki akiwa na umri wa miaka 93.

Nancy Reagan au Nancy Davis, alizaliwa mjini New York tarehe 6 Julai 1921, babake alikua mfanyabiashara na mamake alikua mwigizaji ambaye baadaye aliolewa na daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu. Nancy Reagan alitunukiwa tuzo ya Hollywood akiwa na umri wa miaka 28. Kukutana kwake na Ronald Reagan, ambaye aliachana na mke wake wa kwanza Jane Wyman (mwigizaji), kwa muda wa mwaka mmoja, ilikua mwanzo wa historia ya mapenzi ya zaidi ya nusu karne.

"Kwa siku yangu ya kuzaliwa, alisema Nancy, Ronald Reagan alituma maua kwa mama yangu kwa kumshukuru kuweza kumruhusu kuishi pamoja nami." Katika maisha ya ndoa ya wawili hao, walifaulu kuzaa watoto wawili: Patti, mwaka huo waliofunga ndoa, na Ron mwaka 1958.