MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Kura za mchujo zaanza kupigwa katika majimbo matano

Wafuasi wa Marco Rubio bado wanaamini kuwa watazuia mbio za Donald Trump.
Wafuasi wa Marco Rubio bado wanaamini kuwa watazuia mbio za Donald Trump. RFI/Anne-Maris Capomaccio

Nchini Marekani, wapiga kura wa vyama vya Republican na Democratic wanapiga kura katika uteuzi wa wagombea bora wanaotafuta tiketi ya vyama hivyo kuwania urais mwezi Novemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu umepewa jina la Super Tuesday 2, au Jumanne kuu ya pili kwa sababu uteuzi huo unafanyika katika majimbo matano kwa wakati mmoja ambayo ni pamoja na North Carolina, Ohio, Florida, Illinois na Missouri.

Tayari uteuzi huo umeanza katika baadhi ya majimbo.
Donald Trump wa chama cha Republican na Hillary Clinton wa Democrat wanapewa nafasi kubwa ya kushinda uteuzi wa vyama hivyo.

 

Majimbo matano nchini Marekani yanapiga kura kumteua mgombea atakayewania urais kupitia tiketi ya vyama vyao.

Uchaguzi huo huenda ukawapa fursa wagombea wa vyama vya Democrat na Republican kuimarisha uongozi wao.

Kura zimeanza kupigwa katika jimbo la Ohio na Florida yote yakionekana kuwa muhimu pamoja na majimbo ya Carolina Kaskazini ,illinois na Missouri.

Mgombea wa chama cha Democratic anayeongoza katika chama hicho Hillary Clinton ana imani kwamba atafanikiwa kumuangusha mpinzani wake wa karibu Bernie Sanders.

Kwa upande wake Donald Trump atalenga kuwaangusha wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican.

Bilionea huyo, hata hivyo, anakabiliwa na upinzani katika chama cha Republican pamoja na chama cha Democrats.