BRAZILI-UTEUZI-SIASA

Brazil: Lula ataeuliwa kwenye nafasi ya waziri

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva katika mji wa Buenos Aires.
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva katika mji wa Buenos Aires. REUTERS/Enrique Marcarian

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva ameteuliwa na Rais Dilma Roussef kuwa Waziri Kiongozi wa utawala, nafasi kama ya Waziri Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umetangazwa baada ya siku kadhaa kukabiliwa na mashitaka, huku upinzani ukiendesha hamasa kwa wananchi kwa lengo la kumng'oa madarakani Dilma Rousseff.

Miaka mitano baada ya kuondoka Planalto (ikulu ya rais) kkatika mji mkuu wa Brazili, Brazilia, Lulaamerudi kwa mara nyingine atika ukumbi wa siasa! Baada ya siku kadhaa za mashitaka dhidi yake, Dilma Rousseff amemteua rais wa zamani katika nafasi muhimu ya serikali yake: ile ya Waziri Kiongozi wa utawala, wadhifa muhimu ambapo faili zote zinapaswa kupitia.

Lula amepewa jukumu la kukusanya wabunge wawe karibu na Dilma Rousseff, na kuzuia njia zote kwa utaratibu wa kumtimua rais madarakani, hatua ambayo itaptishwa kwa theluthi mbili ya kura za bunge na baraza la Seneti. Makundi ya wanaharakati wanaompinga Rais Dilma Roussef yamefaulu kuhamasisha watu zaidi ya milioni tatu kuingia mitaani wakati wa maandamano ya Jumapili, mwishoni mwa juma lililopita.

Lakini wakati huo huo, Lula, ambaye hivi karibuni alihusishwa katika matukio kadhaa, anaepuka moja kwa moja kufuatiliwa tena na mahakama za kawaida pamoja na jaji Sergio Moro, ambaye anaendesha kwa mkono wa chuma uchunguzi mkubwa dhidi ya rushwa kwa miaka miwili sasa. Kwa mujibu wa sheria ya Brazil, Lula, kuwa waziri, hatimaye hawezi kuhukumiwa na Mahakama Kuu, hali ambayo itachelewesha mchakato huo.