MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Marekani: Trump na Hillary washinda katika majimbo muhimu

Donald Trump, kati ya mtoto wake Eric (kulia) na meneja wa kampeni zake Corey Lewandowski (kushonto) wakikaribisha matokeo ya kura za mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, North Carolina, Illinois na Missouri (Palm Beach Machi 15, 2016).
Donald Trump, kati ya mtoto wake Eric (kulia) na meneja wa kampeni zake Corey Lewandowski (kushonto) wakikaribisha matokeo ya kura za mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, North Carolina, Illinois na Missouri (Palm Beach Machi 15, 2016). REUTERS/Joe Skipper

Mgombea kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump na mgombea kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton wote wamepata ushindi mkubwa Jumanne hii katika kura za mchujo, ushindi ambao kila mmoja unamruhusu kuimarisha kambi yake.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Donald Trump katika jimbo la Florida umepelekea Marco Rubio, Seneta wa Jimbo hilo, kujiondoa mbio za urais kwa tiketi ya chama cha Republican. John Kasich kwa upande wake amejipatia ushindi wake wa kwanza katika jimbo lake la Ohio.

Hawa hapa ni washindi,jimbo kwa jimbo, katika kura za mchujo za Jumanne hii, kulingana na makadirio ya runinga za Marekani:

- Florida

Republican: Donald Trump

Democratic: Hillary Clinton

- Ohio

Republican John Kasich

Democratic: Hillary Clinton

- North Carolina

Republican: Donald Trump

Democratic: Hillary Clinton

- Illinois

Republican: Donald Trump

Democratic: Hillary Clinton

- Missouri

Republican: bado hawajatanza

Democrats: bado hawajatangaza

- IDADI YA USHINDI -

Democrats:

Hillary Clinton: 4

Bernie Sanders: 0

Republican:

Donald Trump: 3

John Kasich: 1

Ted Cruz: 0

Marco Rubio: 0