BRAZIL-UTEUZI-SIASA

Brazil: Rousseff atetea uamuzi wake

Rais Dilma Rousseff anasema Lula da silva atasaidia kukomboa uchumi wa nchi uliokuwa umeanguka.
Rais Dilma Rousseff anasema Lula da silva atasaidia kukomboa uchumi wa nchi uliokuwa umeanguka. REUTERS/Ueslei Marcelino

Hatimaye Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea uamuzi wake wa kumteua Rais wa zamani wa Brazil, kuwa mkuu wa ofisi yake. Nafasi hii ni sawa na ile ya Waziri Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Rais Dilma Rousseff amebaini kuwa Luiz Inacio Lula da silva ana ujuzi mkubwa na uzoefu wa kisiasa na atasaidia kuimarika kwa hali ya uchumi, uchumi ambo unaendelea kudidimia.

Muda mchache baada ya uteuzi wa Lula da silva, watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanaharakati walikusanyika mbele ya Ikulu ya nchi hiyo, huku wakitumia vipaza sauti wakimtaka Rais Rousseff kujiuzulu kwa kuwa uteuzi wa kiongozi huyo wa zamani ni miongoni mwa njama za kukwepa uchunguzi wa ufisadi unaondelea.

Miaka mitano baada ya kuondoka Planalto (ikulu ya rais) katika mji mkuu wa Brazili, Brazilia, Lula amerudi kwa mara nyingine atika ukumbi wa siasa! Baada ya siku kadhaa za mashitaka dhidi yake, Dilma Rousseff amemteua rais wa zamani katika nafasi muhimu ya serikali yake: ile ya Waziri Kiongozi wa utawala, wadhifa muhimu ambapo faili zote zinapaswa kupitia.

Lula amepewa jukumu la kukusanya wabunge wawe karibu na Dilma Rousseff, na kuzuia njia zote kwa utaratibu wa kumtimua rais madarakani, hatua ambayo itaptishwa kwa theluthi mbili ya kura za bunge na baraza la Seneti. Makundi ya wanaharakati wanaompinga Rais Dilma Roussef yamefaulu kuhamasisha watu zaidi ya milioni tatu kuingia mitaani wakati wa maandamano ya Jumapili, mwishoni mwa juma lililopita.

Lula, ambaye hivi karibuni alihusishwa katika matukio kadhaa, anaepuka moja kwa moja kufuatiliwa tena na mahakama za kawaida pamoja na jaji Sergio Moro, ambaye anaendesha kwa mkono wa chuma uchunguzi mkubwa dhidi ya rushwa kwa miaka miwili sasa. Kwa mujibu wa sheria ya Brazil, Lula, kuwa waziri, hatimaye hawezi kuhukumiwa na Mahakama Kuu, hali ambayo itachelewesha mchakato huo.