BRAZILI-UTEUZI-SIASA

Hali ya kisiasa Brazil yaendelea kudorora

Rais wa zamani wa Brazil Lula alijikua uteuzi wake katika serikali ukisimamishwa na jaji, Machi 17 2016.
Rais wa zamani wa Brazil Lula alijikua uteuzi wake katika serikali ukisimamishwa na jaji, Machi 17 2016. REUTERS/Adriano Machado

Baada ya Lula kuteuliwa katika serikali, Jumatano hii, Machi 16, baada ya kuapishwa kwake Alhamisi hii, hali imeendelea kuwa nguma, kwa sababu jaji wa mahakama ya mwanzo amesimamisha uteuzi huo wa Rais wa zamani.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mwengine serikali imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa jaji wa mahakama ya mwanzo. Wakati huo huo, Wawakili wa raia katika Bunge la Brazil wametoa wito kwa harakati za kung'atuliwa madarakani kwa Rais Dilma Rousseff.

Uamuzi wa jaji wa mahakama ya mwanza wa kufuta uteuzi wa Lula katika serikali ni pigo kubwa kwa rais Dilma Rousseff, lakini ni uamuzi wa muda ambao unaweza kubadilishwa wakati wowote na mgogoro huu wa kisheria unaweza kuendelea. Hali iliendelea kuongezeka umatano jioni wiki hii na Brazil inatumbukia katika mgogoro wa kisiasa. Mazungumzo ya simu yaliosikilizwa na vyomo vya sheria vya Brazili yaliwekwa wazi Jumatano hii jioni, ambapo inaonekana kuwa Rais Dilma Rousseff amempa mtangulizi wake Lula Da Silva njia ya kujilinda na vyombo vya sheria vya Brazil.

Lula hivi karibuni aliteuliwa kwenye nafasi ya waziri, nafasi ambayo ni ya juu katika serikali, sawa na ile ya Waziri Mkuu nchini humo. Inaonekana kwamba kuna tafsiri kadhaa kuhusu mazungumzo hayo kati ya Rais Dilma Rousseff na mtangulizi wake Lulu Da Silva. Rousseff alitumia kauli kali, wakati wa kuapishwa kwa Lula, Jumatano asubuhi. Alisema kwamba viongozi wa mapinduzi hawatomshawishi ili "ageuke katika maamuzi yake au kuwakandamiza raia", wakati ambapo wafuasi wake katika ukumbi wa Ikulu ya rais, walikua wakipiga kelele: "Hakutakuwa na mapinduzi" .

Maelfu ya raia wanaadamana tangu Jumatano nchini kote. Maandamano haya yamesambaa katika miji kadhaa. Katika mji mkuu wa Brasilia, kulitokea makabiliano, jeshi lililazimika kuingilia kati ili kutenganisha wafuasi kutoka kambi mbili. Katika mji wa Sao Paulo, waandamanaji wamekua wakikusanyika mbele ya makao makuu ya makampuni ya serikali ya jimbo la Sao Paulo. Kulionekana bango kubwa lenye maandishi "sasa unatakiwa kujiuzulu".

Serikali yakata rufaa

Wakili Mkuu wa serikali ya Brazil, José Eduardo Cardozo, ametangaza kuwa amekataa rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa mahakama ya mwanzo ambaye alifuta uteuzi wa rais wa zamani Lula Da Silva kama Waziri muhimu wa Rais Dilma Rousseff.

"Hakuna matumizi mabaya ya madaraka" katika uteuzi wa rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva (2003-2010) na "Sababu ya uteuzi wake si wa kumkwepesha dhidi ya uchunguzi" amehakikisha José Cardoso, waziri wa sheria wa zamani wa Rousseff.

Wabunge wataka kumng'atua Dilma Rousseff

Wabunge wameunda kamati maalum ya Wabunge 65, ambao watahusika na kuandaa rasimu ya ripoti inayopendekeza au la muendelezo wa harakati za kung'olewa madarakani zilizoanzishwa dhidi ya rais, anayeshutumiwa na upinzani kujilimbikizia mamilioni ya pesa ya serikali mwaka 2014, mwaka aliyechaguliwa kwa mara nyingine, na mapema mwaka 2015.