MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Barack Obama kuwahutubia Wacuba

Barack Obama na Raul Castro wakipeana mikono kwa muda mrefu katika Ikulu ya Mapinduzi mjini Havana Jumatatu hii, Machi 21 2016.
Barack Obama na Raul Castro wakipeana mikono kwa muda mrefu katika Ikulu ya Mapinduzi mjini Havana Jumatatu hii, Machi 21 2016. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Barack Obama anatazamiwa Jumanne hii kuwahutubia mamilioni ya Wacuba kutoka katikati mwa mji mkuu wa Cuba, Havana, ili kujadili mustakabali wa uhusiano kati ya nchi hizi mbili, uliokua umevunjika kwa kipindi cha nusu karne.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba, inayosubiriwa katika kisiwa hicho, itarushwa hewani moja kwa moja kwenye runinga ya taifa ya Cuba. Desemba 17, 2014, Barack Obama alionekana kwa mara ya kwanza kwenye televisheni za Cuba kutoka White House, akitangaza - kwa mshangao mkubwa - kufufuliwa kwa uhusiano kati ya Marekani na utawala wa kikomunisti.

"Hii ni fursa ya kipekee katika ziara hii ya kuchukua muda fulani na kuongea moja kwa moja na Wacuba wote," amesema Ben Rhodes, mshauri wa karibu wa Bw Obama, ambaye aliongoza mazungumzo ya siri yaliopelekea kufufuliwa kwa mahusiano hayo kati ya nchi hizi mbili, mahusiano ambayo yalikua yalivunjika kwa kipindi cha nusu karne.

Wakati ikisalia miezi kumi ya kuondoka kwake kutoka White House, Bw Obama anataka kuchukua fursa ya hotuba hii kutoka ukumbi wa jengo kubwa la Alicia Alonso, ambao una uwezo wa kupokea watu 1,300, ili kutoa maono yake ya mahusiano kati ya Marekani na Cuba, mapoja na yeye kuondoka White house lakini piamaono ya Raul Castro, ambaye anatazamiwa kustaafu mwaka 2018.

"Nimekuja Havana kufuta masalia ya mwisho ya vita baridi katika Ukanda huu na kuzindua enzi mpya ambayo itasaidia kuboresha maisha ya kila siku ya Wacuba," Obama ameeleza kwenye Facebook.

Baada ya hotuba hii, Obama atakutana na kundi la wapinzani wa Cuba kwenye Ubalozi wa Marekani.

White House inakubali ukosefu wa maendeleo juu ya uhuru wa watu binafsi nchini Cuba tangu mwishoni mwa mwaka 2014. Lakini amehakikisha kuwa atazidisha majadiliano "sahihi na ya moja kwa moja" juu ya sula hili.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu kwa sauti ya kuhamaki, Raul Castro alionekana akijibu kwa hasira mwandishi wa habari wa Marekani ambaye aimuulizwa kuhusu wafungwa wa kisiasa.

"Nipe orodha mara moja ili niwaache huru. Nipe jina au majina. Kama wapo, Niwaache huru kabla ya usiku!" kiongozi wa Cuba amesema.

- Baseball kisha Rolling Stones -

je, White House ina orodha hiyo, na iko tayari kuiwasilisha kwa mamlaka ya Cuba?

Kwa mujibu wa Ben Rhodes, suala hili limekua likijadiliwa mara kwa mara katika mikutano kati ya nchi hizo mbili. "Tatizo si kusema kwamba hawajui kesi hizi lakini hawawachukulii kama wafungwa wa kisiasa," amesema Ben Rhodes.