BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Chama cha mawakili chaomba Roussef kujiuzulu

Rais wa Brazil Dilma Rousseff, anakabiliwa na kashfa ya Rushwa.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff, anakabiliwa na kashfa ya Rushwa. REUTERS/Adriano Machado

Chama cha mawakili nchini Brazil (OAB) kitawasilisha Jumatatu hii ombi jingine la kumtaka Rais wa nchi hiyo kutoka mrengo wa kushoto Dilma Rousseff ajiuzulu, wakati mabapo utaratibu wa kwanza kwa madai ya kupitisha mlango wa nyuma mali ya umma, tayari umejadiliwa na kamati ya Bunge.

Matangazo ya kibiashara

"Mashtaka ipo katika katiba yetu kama suluhu ya kisheria kwa demokrasia yetu," mwenyekiti wa kamati hiyo, Claudio Lamachia, amesema, akiliambia gazeti la O'Globo, akimjibu Rais Dilma Rousseff , ambaye analaani "mapinduzi" ya taasisi dhidi yake.

Kamati ya ndani ya chama cha mawakili (OAB) lilipendekeza mwezi Novemba mwaka jana kwamba haiungi mkono kujiuzulu kwa rais wa Brazili.

Lakini tangu chama hicho kilipopokea "taarifa za Mahakama Kuu na (mahakama ya mwanzo) kuhusu operesheni inayojulikana kwa jina la "Quick Wash", uchunguzi kuhusu mtandao wa rushwa unaoizunguka kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobras, uliendelea kuukabili muungano wa mrengo wa kati kushotoulio madarakani, Bw Lamachia, ameeleza.

"Taasisi yetu, ambayo inatetea na kuendeleza demokrasia imefikia uamuzi uliopitishwa karibu kwa kauli moja (mashirikisho 26 kwa jumla ya 27) kuhusu suala nyeti," Bw Lamachia amesema, "uamuzi wa kiufundi kabisa" na sio wa kisiasa.

Kamati maalum ya wabunge 65 tayari inatathimi, tangu Machi 18, ombi la kwanza kwa mashtaka dhidi ya Rais Dilma Rousseff, kura ya theluthi mbili ya Wabunge kisha ya theluthi mbili ya Maseneta, zinahitajika ili kumtimu madarakani rais huyo mkuu wa nchi.