CUBA-MAREKANI-FIDEL-USHIRIKIANO

Fidel Castro afutilia mbali hotuba ya Obama Cuba

Fidel Castro akishikilia toleo la gazeti ya serikali ya Cuba la Granma la tarehe 19 Oktoba 2012 ambapo alielezwa kuwa aalifariki. Alishutumu mashirika ya habari ya kigeni, kuwa maadui wa Cuba ya kuchapisha taarifa za uongo juu ya hali yake ya afya.
Fidel Castro akishikilia toleo la gazeti ya serikali ya Cuba la Granma la tarehe 19 Oktoba 2012 ambapo alielezwa kuwa aalifariki. Alishutumu mashirika ya habari ya kigeni, kuwa maadui wa Cuba ya kuchapisha taarifa za uongo juu ya hali yake ya afya. REUTERS/Alex Castro/Courtesy of Cubadebate

Aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro, Jumatatu hii, amemuandikia barua rais wa Marekani Rais Barack Obama, akikosoa vikali hotuba yake. Rais Obama alitoa wito kwa mabadiliko katika nchi hiyo ya kikomunisti wakati wa ziara yake ya kihistoria wiki iliyopita mjini Havana.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua hiyo ndefu, yenye kichwa cha habari "ndugu Obama," rais wa zamani wa Cuba, aliyejiondoa madarakani mwaka 2006, amemkebehi Rais Obama kwa hotuba aliyoitoa machi 22, siku ya mwisho ya ziara yake mjini Havana, ziara ambayo ni ya kwanza kwa rais wa Marekani tangu miaka 88

Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana akikosoa ziara hiyo.

Fidel Castro, aliyemkabidhi kakake Raul madara zaidi ya miaka 10 iliyopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka Marekani.

Fidel Castro ametupilia mbali pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika wa kuunda urafiki na kuzika masalio ya Vita Baridi vya barani Amerika, huku akikumbusha kuhusu uvamizi wa Bay of Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na Marekani mwaka 1961.

Amewaonya raia wa Cuba kutoweka akilini ahadi za Rais Obama, na kuwasihi kuwa maeneo yake ni sawa na “rojo ya sukari”, na kuwataka kutoyafuata.