Marekani: milio ya risasi yasikika ndani ya jengo la Congress
Imechapishwa: Imehaririwa:
Majengo ya Congress ya Marekani na White House yamezingirwa Jumatatu hii, Machi 28, kufuatia risasi zilizorushwa katikati ya sehemu ya kupokelea wageni.
Mtu mmoja amekamatwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, ambavyo pia vimearifu kuwa askari polisi mmoja amejeruhiwa.
There has been an isolated incident at the US Capitol. There is no active threat to the public
— DC Police Department (@DCPoliceDept) March 28, 2016
"Tukio limezimwa katika Makao Makuu ya Baraza la wawakilishi na Baraza la Seneti (Capitole). Hakuna tishio dhidi ya raia," polisi ya mji wa Washington DC imeandika kwenye Twitter.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka marekani (polisi, vyombo vya habari), mshambuliaji amejeruhiwa kisha amesafirishwa hospitalini. Hata hivyo kuna askari polisi ambaye amejeruhiwa, lakini si sana.
Capitole, jengo la Baraza la Seneti na Baraza la
Shelter in place remains in effect as Capitol Police continue to investigate. Please stay in your assigned location. #alert
— SenateSergeantAtArms (@SenateSAA) March 28, 2016
Wawakilishi, kwa sasa wakiwa likizo kwa ajili ya Pasaka, bado limezingirwa "wakati ambapo polisi ya Capitole ikiendelea na uchunguzi," polisi ya Baraza la Seneti, hata hivyo, imeandika kwenye twitter, U.S. Senete Sergeant at Arms Office.
Ujumbe wa ndani uliopita kwa Capitol umeonyesha kuwa majengo yalikua "yamezingirwa kufuatia taarifa kuhusu risasi zilizorushwa katikati ya sehemu wanakopokelea wageni." Ikulu ya White House pia imefungwa, wafanyakazi wamepigwa marufuku ya kuingia au kutoka.