BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Brazil: muungano wa Dilma Rousseff karibu kulipuka

Makamu wa Rais Michel Temer na Rais Dilma Rousseff, Desemba16, 2015.
Makamu wa Rais Michel Temer na Rais Dilma Rousseff, Desemba16, 2015. EVARISTO SA / AFP

Sherehe ya Pasaka ilikuwa fupi kwa Rais wa Brazil Dilma Rousseff. Rais Rousseff anaekabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, na ambaye anakabiliwa na tishio la utaratibu wa kujiuzulu, anaweza kujikuta muungano wakeunavunjika wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Jumanne Machi 29, chama cha mrengo wa kati katika Bunge cha PMDB na mshirika mkuu wa muungano utawala, unatarajiwa kuondoka rasmi serikalini.

Chama cha mrengo wa kati cha PMDB chenye Wabunge 69, ni chama kikuu chenye Wabunge wengi katika Bunge la Brazil. Bila kuungwa mkono na chama hiki, rais atakau an matatizo ya kuongoza nchi hiyo. Kuna hatari vyama vingine washirika wa muungano vinaweza kufuata hatua ya chama cha PMDB. Kiongozi wa chama cha PMDB ni Makamu wa Rais wa nchi, Michel Temer, mtu mwenye busara ambaye tayari anajiandaa kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi iwapo Dilma Rousseff atajiuzulu.

Kwa miezi kadhaa chama cha PMDB kimefuta imani kwa Rais Dilma Rousseff. Mwezi Oktoba mwaka jana, chama hicho kiilipitisha "mpango wa serikali" wa uongozi huria. Rais Dilma Rousseff ameanzisha harakati za kuwashawisi wabunge kutokana na tishio la kujiuzulu.

Harakati hii ni ya kuzuia chama idadi ya theluthi mbili zinahitajika kuanzisha mchakato wa wa kujiuzulu. Kazi ambayo rais amemkabidhi mtangulizi wake na mshauri wake mkuu Lula Da Silva. Pamoja na tuhuma za rushwa dhidi yake, mwanzilishi wa chama cha Wafanyakazi anatumia nguvu zake zote ili kuokoa si tu Dilma Rousseff, lakini pia urithi wa chama cha PT.

Lula Da Silava ametolea wito wafuasi wake kuingia mitaani ili kulaanikile ambacho Rais wa Brazil anataja kuwa ni jaribio la "mapinduzi". Maandamano ya kumuunga mkono Dilma Rousseff yamepangwa kufanyika Alhamisi wiki hii.