MAREKANI-SHAERIA-OBAMA

Obama apunguza adhabu za wafungwa 61

Rais wa Marekani Barack Obama akimsalimu mfungwa wa zamani mjini Washington, Machi 30, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama akimsalimu mfungwa wa zamani mjini Washington, Machi 30, 2016. NICHOLAS KAMM/AFP

Rais wa Marekani Barack Obama, Jumatano hii, amepunguza adhabu zilizokua zikiwakabili wafungwa 61 waliohukumiwa kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya. Hili ni tukio la kihistoria wakati ambapo amekua akishawishi wahusika katika sekta ya sheria kufanya mageuzi ya kijinai kuhusu makosa madogo madogo.

Matangazo ya kibiashara

Obama amepunguza adhabu za wafungwa 61, waliokua wamehukumiwa kuanzia kifungo cha maisha hadi adhabu ndogo ndogo gerezani kwa kumiliki au kuuza madawa ya kulevya kama Crak au cocaine, Ikulu ya White House imetangaza.

Barack Obama, ambaye anafikia mwishoni wa muhula,amekua akizidisha juhudi kama hizi. Mwezi Desemba, alipunguza adhabu kwa wafungwa 95 wa Marekani.

Hivi karibuni alipunguza adhabu kwa wafungwa 248 waliohukumiwa, na baadhi yao walipewa msamaha, na Jumatano hii anatazamiwa kukutana na wafungwa wengine.

Rais wa Marekani, kwa muda mrefu, amekua akiomba mageuzi ya sheria za jinai, akilaani jinsi magereza yamekua yakijaa wafungwa na hivo kusababisha vitendo viovu sugu, kutokana na kuzuiliwa kwa kipindi kirefu katika magereza.

Bw Obama alitoa mfano wa ahadi yake ya mageuzi kwa kutembelea mwezi Julai katika jela moja nchini Marekani, ikiwa tukio la kwanza kuwahi kutokea kwa Rais aliye madarakani nchini Marekani.

Watu milioni 2.2 wanazuiliwa katika magereza tofauti nchini Marekani na Rais Obama amesema akisisitiza kwamba Wamarekani wanawakilisha "5% ya idadi ya watu duniani, lakini 25% ya watu wanaozuiliwa gerezani duniani", ikiwa ni pamoja na watu weusi na watu kutoka jamii ya Hispanics.

Miongoni mwa watu wanaozuiliwa gerezani nchini Marekani, zaidi ya nusu walihukumiwa kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya, imebaini mwezi Oktoba tathmini ya Idara ya Takwimu ya vyombo vya sheria iliyofanywa mwaka 2012 katika sampuli ya mahabusu 94,678.