MAREKANI-TRUMP-SIASA-SHERIA

Uchaguzi Marekani: Donald Trump amtetea mshauri wake

Mgombea kwa tiketi ya chama cha  Republican Donald Trump wakati wa hotuba yake katika mji wa Janesville, Wisconsin, Machi 29, 2016.
Mgombea kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump wakati wa hotuba yake katika mji wa Janesville, Wisconsin, Machi 29, 2016. REUTERS/Kamil Krzaczynsk

Meneja wa Kampeni za mwasiasa wa chama cha Republocan nchini Marekani Donald Trump, amefunguliwa mashhtaka ya kumvamia na kumjeruhi mwandishi wa Habari wakati wa mkutano wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump haraka amelaani uamuzi huo na kusema kuwa ana mashaka na uhalali wa malalamiko ya mshitaki wake.

Corey Lewandowski, ambaye aliripoti kwa hiari yake

mbele ya polisi ya Jupiter katika mji wa Florida, amefahamishwa kuripoti Mei 4 kwa tuhuma za kumvamnia na kumjeruhi mwanahabari Michele Fields, ambaye alijaribu kumhoji Donald Trump baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu klabu yake ya gofu mjini Florida, Machi 8.

Hata hivyo Corey Lewandowski amekanusha tuhuma dhidi yake.
Polisi wanasema wana mkanda wa Video unaothibitisha kuvamiwa kwa mwanahabari huyo.

Meneja huyo anatarajiwa kufikishwa tena Mahakamani hivi karibuni.