PERU-FUJIMORI

Mahakama ya Katiba yatupilia mbali rufaa ya Fujimori

Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori katika mahakama ya Lima,Julai 20, 2009.
Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori katika mahakama ya Lima,Julai 20, 2009. (Photo: Reuters)

Mahakama ya Katiba (TC) ya Peru imekataa ombi la Rais wa zamani Alberto Fujimori kufuta hukumu yake ya miaka 25 jela kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu", chanzo kilio karibu na kesi hii kimeliambia shirika la habri la AFP Jumanne hii Mei 3.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa TC walikutana kwa muda wa saa tatu na hatimaye walitupilia mbali kwa kura sita dhidi na ya moja kwa rufaa iliyowasilishwa wanasheria wa rais wa zamani katika utawaa wa udikteta, Alberto Fujimori. Mwanasheria wake, William Paco Castillo, alikua tayari alitangaza kwamba atawasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama za kimataifa, kama vile mahakama ya haki za binadamu ya Amerika, iwapo atashindwa siku ya Jumanne.

Alberto Fujimori, madarakani kati ya mwaka 1990 na 2000 na sasa ana umri wa miaka 77, alipatikana na hatia ya kuagiza mauaji mara mbili yalioyotekelezwa na kikosi chake mwaka1991 na 1992, kama sehemu ya mapambano dhidi ya waasi wa Mao. Wakati huo watu ishirini na tano waliuawa.

Bw Fujimori alikua ameiomba Mahakama ya Katiba kufuta hukumu yake, kuandaa kesi mpya na kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo. Ilikuwa rufaa ya mwisho inayowezekana nchiniPeru kwa rais wa zamani, ambaye alikuwa tayari amewasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama mbalimbali nchini humo, bila mafanikio. Aliposikilizwa kwa njia ya simu katika Mahakama ya Katiba, Fujimoro amejitetea akisema kuwa hana hatia.

Rais huyo wa zamani wa Peru anazuiliwa tangu mwaka 2007 katika kambi ya polisi mashariki mwa mji wa Lima.

Mwanasheria wake, Paco Castillo, alikua alisema katika kukata rufaa kuwa kesi hiyo iligubikwa na ukosefu wa uadilifu katika mahakama ya mwanzo, utaratibu ambao ulimalizika kwa kumuhukumu mteja wake. Tangu 2013, Bw Fujimori alitafuta kuhukumiwa upya, akiweka mbele ukosefu wa uadilifu katika kesi yake mahakami. Fujimori alikua na imani kuwa huenda adhabu yake ingelipunguzwa.