MAREKANI-OBAMA-HIROSHIMA

Ziara ya kihistoria ya Obama Hiroshima

Rais wa Marekani Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 6 Mei 2016 katika Ikulu ya White House.
Rais wa Marekani Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 6 Mei 2016 katika Ikulu ya White House. REUTERS/Carlos Barria

Barack Obama atazuru mji wa Hiroshima Mei 27 katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Japan.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza kwa rais wa Marekani kwenye eneo kulikotokea mlipuko wa bomu la kwanza la atomiki lililorushwa Agosti 6,1945 na kuua watu 140,000. Ikulu ya White House inasema haimaanishi kuwa Barack Obama ataomba msamaha.

Ziara hii ya kihistoria inaandaliwa kwa miezi kadhaa sasa. Ingawa Barack Obama hajawahi kuomba msamaha wakati wa ziara yake Hiroshima, uwepo wake kwenye eneo kulikotokea mlipuko wa kwanza wa bomu la atomiki unaweza kutafsiriwa kwa maoni mbalimbali nchini Marekani. Kwa mujibu wa Ikulu ya White House, rais wa Marekani atatoa hotuba akionyesha ahadi yake kwa dunia isiyokua na silaha ya nyuklia.

Akitembelea Hiroshima mwezi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, alifungua njia kwa baraka za rais. Zoezi hili pengine litakaribishwa kimataifa, lakini ni hatari katika suala la sera za ndani kwa Barack Obama, ambaye ataondoka Ikulu ya White House mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa upande wake, chama Republican ambacho kinaendelea na kampeni zake za uchaguzi wa urais, kwa miezi kadhaa kimekua kikimkosoa "rais ambaye amedhoofisha Marekani kwa kuomba msamaha."

Obama atajitahidi kutumia maneno mazuri ili asiwezi kuwakosea maveterani wa Marekani waliopigana katika vita vya Marekani dhidi ya Japan.