VENEZUELA-OAS-MVUTANO

Mkuu wa OAS amtaja Nicolas Maduro "dikteta hatari"

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro atangaza hali ya hatari.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro atangaza hali ya hatari. Miraflores Palace

Nchini Venezuela, upinzani unaendelea kudai kufanyika kwa kura ya maoni ili kumuondoa mamlakani Rais Nicolas Maduro, mpango ambao viongozi wa Venezuela wamefutilia mbali.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi ambao umesababishwa Jumuiya ya nchi za Amerika (OAS) kutoa msimamo usio kuwa wa kawaida.

Katibu Mkuu wa sasa wa Jumuiya ya nchi za Amerika(OAS), Luis Almagro haina kutoka Uruguay hakuficha msimamo wa Jumuiya hiyo. Katika barua aliyoandika amemtaja Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kuwa ni "msaliti".

Rais Nicolas Maduro amekataa kata kata kufanyika kwa kura ya maoni kwa lengo la kumng'oa mamlakani. Badala yake, Rais Maduro ametangaza hali ya hatari. Kwa upande wake, hali ya sasa ni kutokana na "vita vya kiuchumi" viliyosababishwa na viongozi wa mrengo wa kulia.

Hata hivyo, machafuko yamekua yakiibuka kila kukicha nchini kote tangu kuanguka kwa bei ya mafuta ambayo yanaingiza katika hazina ya serikali 96% ya sarafu ya nchi hiyo. Raia kwa sasa na uhaba wa chakula kama vile sukari, mkate, mchele. Venezuela inakabiliwa na kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei duniani: zaidi ya 180% mwaka 2015.

"Mimi si afisa wa Idara ya Ujasusi (CIA), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Amerika amemuandikia Rais wa Venezuela, akimshtumu kukataa kuonana na raia, kukataa kuwapa nafasi ya kufanya uamuzi, na hivyo kuwa dikteta hatari, kama wale wote waliowahi kuishi katika bara hili. "