MAREKANI-CLINTON-TRUMP

Hillary Clinton amshambulia kimaneno Trump

Hillary Clinton na Donald Trump wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kura za mchujo katika majimbo matano yanayosalia kwa «Jumanne Kuu», Aprili 26, 2016. 2016.
Hillary Clinton na Donald Trump wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kura za mchujo katika majimbo matano yanayosalia kwa «Jumanne Kuu», Aprili 26, 2016. 2016. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files

Bi Hillary Clinton anayegombea tiketi ya kuwania urais nchini Marekani kupitia chama cha Democratic anasema mgombe wa chama cha Republican Donald Trump ni mtu hatari ambaye hawezi kuaminiwa na hivyo hawezi kuwa rais.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa hao wawili ambao wanapewa nafasi kubwa kupambana katika kinyanganyiro cha mwezi Novemba, siku za hivi karibuni wameonekana wakivamiana na kukosoana hadharani.

Bi Clinton amesisitiza kuwa, Bwana Trump ikiwa atakuwa rais atakosa mbinu na uelewa wa kuwaleta pamoja washirika wa Marekani.

Trump naye amekuwa akimshutumu Clinton na mumewe Bill Clinton ambaye aliwahi kuwa rais wa Marekani kwa namna alivyoongza nchi hiyo.