MAREKANI-HIROSHIMA-OBAMA

Obama hatoomba msamaha kwa bomu la atomiki Hiroshima

ais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano na waandishi wa habari, le Aprili 5, 2016.
ais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano na waandishi wa habari, le Aprili 5, 2016. REUTERS/Gary Cameron

Barack Obama, ambaye Ijuma wiki hii atafanya ziara ya kwanza ya rais wa Marekani alioko madarakani katika mji wa Hiroshima, ulioshambuliwa kwa bomu la atomiki na Marekani mwaka 1945, ameliambia shirika la serikali la utangazaji la Japan NHK kuwa hatoomba msamaha katika tukio hilo.

Matangazo ya kibiashara

"Hapana, kwa sababu nadhani ni muhimu kutambua kuwa katika vita, viongozi wanapaswa kuchukua kila aina ya maamuzi," Bw Obama amesema alipokuwa akijibu swali la kujua kama atauomba msamaha.

"Ni kazi ya wanahistoria ya kuuliza maswali na kuyachunguza lakini najua, kuwa mwenyewe niko nafasi hii kwa miaka saba na nusu, kila kiongozi huchukua maamuzi magumu sana, hasa katika wakati wa vita" , Obama ameongeza katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu hii na shirika la utabgazai la NHK.

Katika utafiti wa shirika la habari la Japan la Kyodo uliofanywa kwa manusura 115 wa mashambulizi ya mabomu ya atomia mjini Hiroshima asubuhi ya Agosti 6, 1945 na Nagasaki siku tatu baadaye, karibu 80% (78.3%) wanasema kutoomba msamaha wakati 15.7% wangependa kusikia maneno hayo kutoka kwa rais wa Marekani, kwa mujibu wa uchaguzi uliyotolewa Jumapili.

Obama anatazamiwa kuutembelea mji wa Hiroshima tarehe 27 baada ya mkutano wa marais na viongozi wa serikali za G7 katika mji wa Ise-Shima katikati mwa Japan. Ikulu ya White House ilionya kuwa rais, ambaye hatotoa hotuba halisi lakini maneno machache tu, ataacha mjadala juu ya uhalali wa matumizi ya silaha za atomiki utakaoendeshwa na Harry Truman kwa wanahistoria. Lengo litakua kwanza kuthibitisha ahadi yake ya mipango ya dunia bila silaha za nyuklia.

Haijaeleweka kuhusu ratiba maalum ya ziara hiyo na mkutano unaowezekana kati ya rais Obama na Hibakusha (manusura wa bomu la atomiki).

Mashambulizi dhidi ya mji wa Hiroshima yaliyowaua (watu 140,000) na Nagasaki (watu 74,000) siku tatu baadaye yalisababisha Japan kujisalimisha na mwisho wa Vita Kuu vya pili vya dunia.

Rais Barack Obama na mwenzake wa Vietnamese Tran Dai Quang Mei 23, 2016 katika Ikulu ya rais Hanoi.
Rais Barack Obama na mwenzake wa Vietnamese Tran Dai Quang Mei 23, 2016 katika Ikulu ya rais Hanoi. AFP

Hayo yakijiri Rais wa Marekani Barack Obama amesema Jumatatu kuwa anataka "kuimarisha uhusiano" kati ya nchi yake na Vietnam, siku ya kwanza ya ziara yake mjini Hanoi ambayo inaonekana kama ishara ya nguvu iliyotolewa kwa nchi jirani ya China.

"Ujio wetu ni ishara ya kuimarisha mahusiano ambayo tuliyofufuai katika miongo ya hivi karibuni," Obama amesema wakati wa mkutano na Rais Vietnam, Tran Dai Quang.