VENEZUELA-MAANDAMANO

Venezuela: Upinzani watoa wito kwa maandamano mapya

Upinzani nchini Venezuela unatazamiwa kuandamana Jumatano hii ili kuongeza shinikizo kwa serikali ya Kisoshalisti na kumshinikiza Rais Nicolas Maduro kuondoka haraka mamlakani.

Rais Nicolas Maduro Mei 16, 2016 Caracas.
Rais Nicolas Maduro Mei 16, 2016 Caracas. JUAN BARRETO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Venezuela wamejawa na hasira kutopkana na hali ya kiuchumi ambayo imeendelea kudoroa na kusababisha hali ngumu ya maisha nchini humo.

Muungano wa vyama viliyo na wabunge wengi (MUD) umekua ukiandaa maandamano kwa wiki kadhaa sasa, na umeahidi kuhakikisha umemng'a mamlakani Rais Nicolas Maduro. Muungano huo hivi karibuni ulitangaza kwamba utaandaa kura ya maoni ifikapo Januari 10 mwakani kwa minajili ya kumtimua madarakani Rais Nicolas Maduro, mwenye umri wa miaka 53. Rais Maduro, iwapo atatimuliwa madarakani, bila shaka atarejelewa kwenye nafasi yake na Makamu wake.

Muungano huo wa vyama viliyo na wabunge wengi (MUD) kwa sasa, umewataka wafuasi wake kuandamana mbele ya mahakama ya miji mikubwa ya Venezuela, ili kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama Kuu (TSJ).

Hata hivyo Mahakam Kuu imekataza uhamasishaji dhidi ya Baraza la kitaifa la Uchaguzi (CNE), linalohusika na kukagua saini milioni mbili ziliyowasilishwa mapema mwezi Mei na upinzani wa mrengo wa kati-kushoto, hatua ya kwanza ya mchakato mrefu kuelekea kura ya maoni.

"Kwetu sisi uamuzi huo haupo," amepinga mbunge Julio Borges, kiongozi wa wa muungano wa MUD Bungeni, huku akitangaza kwamba, Alhamisi wiki hii, maandamano yatafanyika mbele ya ofisi za CNE, ili iweze kuongeza kasi kwa kazi yake.