MAREKANI-BARACK OBAMA

Obama kutohudhuria mazishi ya Ali

Mwanamasumbwi Muhammad Ali aliyefariki dunia juma lililopita.
Mwanamasumbwi Muhammad Ali aliyefariki dunia juma lililopita. Reuters/路透社

Rais wa Marekani Barack Obama hatahudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa bingwa wa dunia katika mchezo wa masumbwi Muhammad Ali siku ya Ijumaa, aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya marekani inasema, Obama na mkewe Mitchel watakuwa katika shughuli nyingine ya kuhudhuria mahafali ya Binti yao Malia.

Hata hivyo, wameandika barua itasomwa kwa familia ya Mohammad Ali.

Viongozi wa dunia wakiwemo rais Recep Tayyip Erdogan, Mfalme wa Jordan Abdullah wataungana na maelfu ya raia wa Marekani kumwaga mwanmasumbwi huyo katika mji wa Kentucky alikozaliwa.