MAREKANI-CLINTON-SANDERS

Sanders ashinikizwa kumuunga mkono Hillary Clinton

Wagombea urais katika kura za mchujo kutoka chama cha Democratic Bernie Sanders na Hillary Clinton, Machi 9, 2016 wakati wa mjadala katika mji wa Kendall katika jimbo la Florida.
Wagombea urais katika kura za mchujo kutoka chama cha Democratic Bernie Sanders na Hillary Clinton, Machi 9, 2016 wakati wa mjadala katika mji wa Kendall katika jimbo la Florida. REUTERS/Carlo Allegri

Mwanasiasa wa chama cha Democratic Bernie Sanders anayetafuta tiketi ya chama hicho kuwania urais mwezi Novemba, ameanza kupata shinikizo za kuachana na harakati hizo na badala yake kumuunga mkono Bi Hillary Clinton.

Matangazo ya kibiashara

Bi Hillary clinton tayari amepata wajumbe wanaohitajika kushinda tiketi hiyo.

Sanders amesema atapambana hadi mwisho kuelekea uteuzi katika jibo la Washington DC wiki ijayo.

Baadaye hivi leo anatarajiwa kukutana na rais Barack Obama ambaye tayari ameshasema anamuunga mkono Bi Clinton.