MAREKANI

Meya wa Orlando: Marekani haitarudi nyuma, vita dhidi ya IS

Meya wa Florida, Rick Scott
Meya wa Florida, Rick Scott REUTERS/Kevin Kolczynski

Kundi la kiislamu la Islamic State limekiri kuhusika kwenye shambulio la mjini Orlando ambako watu zaidi ya 50 wameuawa, kwenye tangazo lililosomwa redio na mmoja wa makanda wake. 

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya kundi hilo imesema kuwa "Mungu ameruhusu Omar Mateen, mmoja wa wanajeshi wetu nchini Marekani, kutekeleza shambulio hili kwa kuvamia ukumbi wa starehe mjini Orlando, Florida, akiua na kujeruhi wengine zaidi ya 100." ilisema taarifa hiyo.

Kundi la islamic State limeanzisha dola ya kiislamu nchini Iraq na Syria mwaka 2014.

Omar alivamia klabu ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, na kuanza kuwafyatulia risasi mamia ya watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla ya yeye mwenyewe kuuawa.

Wananchi na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja wakiwa wamekusanyika mjini Beaubourg, Paris baa ya shambulio la Orlando.
Wananchi na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja wakiwa wamekusanyika mjini Beaubourg, Paris baa ya shambulio la Orlando. GEOFFROY VAN DER HASSELT / AFP

Vyombo vya usalama nchini Marekani vimemtaja mtuhumiwa kama ni Omar Mateen, raia wa Marekani ambaye kabla ya kutekeleza shambulio hili, alipiga siku kwenye idara ya dharula ya polisi na kusema yeye ni mfuasi wa kundi hilo.

Polisi mjini Orlando imetangaza majina ya watu 22 waliouawa kwenye tukuo hilo na kwamba wataendelea kutoa orodha zaidi ya watu waliouawa na kujeruhiwa.

Saa chache baada ya tangazo la rais Barack Obama kulaani shambulio hili, wagombea urais wa Democratic, Hillar Clinto na Bernie Sander sambamba na wa Republican, Donald Trump, wameungana na kauli ya rais Obama kulaani shambulio hili.

Shirika la ujasusi nchini Marekani, FBI, limekiri kuwa liliwahi kumuhoji, Mateen aliyezaliwa na wazazi raia wa Afghanistan jijini New York, aliachiwa baada ya kuhojiwa na kubainika hakuhusika na shambulio lolote la bomu nchini Marekani.