MAREKANI-OBAMA-ORLANDO

Barack Obama kutembelea Orlando

Watu wakiwasha mishumaa kwa kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la Orlando, Florida, Marekani, Juni 12, 2016.
Watu wakiwasha mishumaa kwa kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la Orlando, Florida, Marekani, Juni 12, 2016. REUTERS/Dylan Martinez

Rais Barack Obama anatarajiwa kusafiri kwenda katika mji wa Orlando Alhamisi wiki hii kwa kutoa heshima kwa wahanga wa shambulio baya lililoendeshwa katika ardhi ya Marekani tangu Septemba 11, Ikulu ya White House ilisema jana Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Rais "atatoa heshima kwa familia za wahanga na atanyesha mshikamano wake na jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ambayo imewapoteza jamaa zao," taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imebaini, baada ya mauaji katika klabu ya mashoga mjini Florida ambapo mshambuliaji kutoka kundi la Islami State aliwaua watu 49 na kuwajeruhi wengine 53.

"Kitendo cha ugaidi na kitendo cha chuki"

Rais Wa Marekani Barack Obama alisema kwa ufupi Jumapili juu ya mauaji ya Orlando yaliyotekelezwa na kijana wa miaka 29. mwenye asili ya Afghanistan, Omar Mateen, akitaja kitendo hicho kuwa ni "cha ugaidi na kitendo cha chuki."

Rais Obama alirejelea tukio hilo jana Jumatatu, katika mkutano na waandishi wa habari. Alibaini kwamba mshambuliaji, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchunguzi aliendesha kitendo hicho peke yake kwa ushawishi "wa vyanzo vya habari vya magaidi kwenye mitandao."

Rais Obama alifutilia mbali, katika hatua hii ya uchunguzi, dhana kwamba shambulizi hilo liliongozwa kutoka nje ya nchi.