COLOMBIA-FARC

Mwisho wa vita viliyodumu muda mrefu Colombia

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (kushoto) na kiongozi mkuu wa waasi wa FARC Timoleon Jimenez, wakizungukwa na Rais wa Cuba Raul Castro.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (kushoto) na kiongozi mkuu wa waasi wa FARC Timoleon Jimenez, wakizungukwa na Rais wa Cuba Raul Castro. REUTERS/Alexandre Meneghini

Serikali ya Colombia na waasi FARC Alhamisi hii wametia saini kwenye mkataba wa kudumu wa kihistoria mjini Havana kuhusu usitishwaji wa mapigano na kuwapokonya silaha waasi, na hivyo kufungua njia kwa azimio la haraka kwa vita viliyoikumba nchi hiyo kwa zaidi nusu karne.

Matangazo ya kibiashara

"Leo ni siku ya kihistoria kwa nchi yetu (...) tumesitisha vita na kundi la waasi wa FARC", Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amekaribisha hatua hiyo, baada ya kumpa mkono kiongozi mkuu wa waasi wa FARC, Timoleon Jimenez, huku wakihudhiria marais kadhaa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Makubaliano haya yataanza kutekelezwa baada ya kutiliwa saini kwenye mkataba wa amani, nchini Colombia, ambapo tarehe haikutajwa. Mkataba huo unaeleza utaratibu wa "kuweka chini silaha, kuhakikishiwa usalama (kwa waasi) na mapambano dhidi ya makundi ya wahalifu" baada ya mazungumzo yaliofanyika kwa miaka mitatu na nusu nchini Cuba.

Vita nchini Colimbia kati ya jeshi na waasi wa FARC vilisababisha vifo vya watu 260,000, watu 45,000 walitoweka na wengine milioni 6.9 waliyahama makazi yao.

Takriban wapiganaji 7000 wa kundi hili la waasi lililoanzishwa mwaka 1964 watawekwa katika maeneo 23 ambapo watalindiwa usalama wao, na watakabidhi silaha zao kwa maafisa wa Umoja wa Mataifa watakaotumwa Colombia mara tu baada ya mkataba wa amani kutiliwa saini.