UN-UNSC

Sweden, Ethiopia na Bolivia zachaguliwa katika Baraza la Usalama la UN

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Desemba 17, 2015.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Desemba 17, 2015. REUTERS/Mike Segar

Sweden, Bolivia na Ethiopia zimechaguliwa Jumanne hii kuwa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kura ya Mkutano Mkuu. Kuna viti viwili kati ya vitano vilioachwa wazi, ambapo wagombea ni Italia na Uholanzi upande mmoja na Thailand na Kazakhstan upande mwingine.

Matangazo ya kibiashara

Nchi zitakazochaguliwa zitashikilia nafasi hizo Januari 1, 2017 kwa kipindi cha miaka miwili.

Kura imepangwa kwa misingi ya kikanda.

Bolivia na Ethiopia zikipasishwa kabla ya kuchaguliwa na makundi yao husika kikanda na hazikuwa na washindani. Bolivia imepata kura 183 na Ethiopia kura 185 kwa jumla ya nchi wanachama 193 wa Bunge.

Italia, Uholanzi na Sweden wamekua wakishindania viti viwili vilikua viliwekewa Ulaya Magharibi.

Italia, ambayo ilikua ikipewa nafasi nzuri ya kushinda katika kura hizi imepata kura 113 tu, Uholanzi imepata kura 125 na Sweden imepata kura 134, wakati wambapo wingi wa kura uliokua unahitajika ilikua kura 128 kwa uchaguzi huu.

Duru nyingine inahitajika ili kuamua kati ya Roma na Hague.

Kazakhstan na Thailand walikua wakishindania kiti kuliyokua kimepewa ukanda wa Asia-Pacific lakini hazikuweza kufaulu, baada ya Kazakhstan kupata kura 113 na Thailand kura 77.

Wagombea - hata wale wasio na washindani -wanapaswa kushawishi theluthi mbili ya wanachama wanaopiga kura wa Mkutano Kuu.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liina wajumbe 15, ikiwa ni pamoja na watano wa kudumu (Marekani, Ufaransa, Urusi, China, Uingereza) ambazo zna kura ya turufu.

Wanachama watano wasio wa kudumu wanachaguliwa kila mwaka. wanahudumu kuanzia Januari 1, na kuendelea kwa kipindi cha miaka miwili.