MAREKANI-GEORGE WASHINGTON

Marekani yaadhimisha miaka 240 ya uhuru wake

Chombo cha kinyuklia cha Marekani cha kubeba ndege George WashingtonJulai 25, 2010.
Chombo cha kinyuklia cha Marekani cha kubeba ndege George WashingtonJulai 25, 2010. Photo : Jo Jung-Ho/Yonhap/ Reuters

Raia wa Marekani leo wanaadhimisha siku ya Uhuru waliopata miaka 240 iliyopita. Mwaka 1776, majimbo mbalimbali ya Marekani yalijikomboa kutoka kwa wakoloni wa Uingereza na baadaye kuungana kuwa nchi moja.

Matangazo ya kibiashara

Wamarekani wanatumai siku hii kukukumbuka kumalizika vita vya mapinduzi lakini pia kukumbuka juhudi za kidemokrasia ilizopiga miaka 200 iliyopita.

Marekani inaendelea kujivunia kuwa mfano wa demokrasia duniani.

Vita vya Uhuru wa Marekani vilipigwa kati ya Uingereza na walowezi wa makoloni yake 13 kwenye pwani ya Amerika ya Kaskazini katika miaka 1775 hadi 1783.

Jeshi la walowezi lililoongozwa na George Washington na wengineo lilishinda jeshi la Dola la Uingereza kwa msaada wa Ufaransa.

Hivyo hatimaye makoloni hayo yakapata uhuru kama “Muungano wa Madola ya Amerika" au Marekani.

Vita na uhuru

Sasa vita kamili vilisambaa. Mwanzoni Waingereza walikuwa na silaha na wanajeshi wengi zaidi, wakasonga mbele, lakini wanamgambo wa walowezi wakioongozwa na George Washington waliendelea kuwashambulia.

Tarehe 4 Julai 1776 wawakilishi kutoka makoloni yote walitangaza uhuru wa Muungano wa Madola ya Amerika. Bado Waingereza walisonga mbele wakatwaa pia mji wa New York.

Lakini tangu mwaka 1777 Ufaransa ulianza kwa siri kutuma silaha kwa Wamarekani; mwaka 1778 Ufaransa, Hispania na Uholanzi ziliungana na kutangaza vita dhidi ya Uingereza. Manowari za Ufaransa zilishambulia meli za Waingereza zilizopeleka silaha na askari kwenda Marekani.

Mwaka 1781 sehemu kubwa ya jeshi la Uingereza lilishindwa kwenye mji wa Yorktown likalazimika kujisalimisha.

Tangu siku hiyo mapigano yalipungua na mwaka 1783 Uingereza ikakubali uhuru wa makoloni yake ya awali.

Wakazi wengi wa makoloni walioendelea kusimama upande wa Uingereza walihamia Kanada iliyobaki kuwa koloni.