MAREKANI-MAUAJI

Video ya mtu mweusi aliyepigwa risasi na polisi yazua mtafaruku

Nchini Marekani, mtu mwengine mweusi ameuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Minnesota na polisi wakati wa ukaguzi wa polisi, Jumatano, Julai 6, siku mbili baada ya tukio kama hilo katika jimbo la Louisiana.

Une manfiestation à Minneapolis, le 30 mars dernier, contre la décision de justice ayant relaxé les deux officiers qui avaient tiré sur une jeune Afro-américain.
Une manfiestation à Minneapolis, le 30 mars dernier, contre la décision de justice ayant relaxé les deux officiers qui avaient tiré sur une jeune Afro-américain. Stephen Maturen / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mpenzi wake amerekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkononi. Video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii imezua hasira leo Alhamisi, na kusababisha wimbi jipya la hasira katika jumuiya ya Wamarekani weusi.

Video ni ya kushangaza. Mwanamke mweusi alikua kwenye uskani wa gari lililokamatwa, huku akirekodi tukio hilo.Alikua karibu na mpenzi wake aliyepigwa risasi na askari polisi. Askari polisi alikua bado akishikilia bunduki, huku akiwa na wasi wasi.

Mtu aliyepigwa risasi alikua katika gari lake na alitaka kuonyesha kitambulisho chake cha uraia wakati askari polisi alipompiga risasi.

"Nilimwambia aonyeshe mikono yake," amesema askari polisi. Mwanamke aliyeona tukio, alijibu: "Ulimtaka aonyeshe leseni yake ya kuendesha gari. Ulimpiga risasimara nne wakati ambapo alikua akionyesha vitambulisho vyake vya uraia. "

Mamia ya watu kwa siku ya pili leo wamekuwa wakiandamana katika mji wa Baton Rouge katika jimbo la Louiziana kulaani kitendo cha afisa wa polisi, kumpiga risasi na kumuua mwanaume mweusi, Alton Sterling.

Wakiwa wamebeba mabango, waandamanaji hao wengi wao wakiwa Wamarekani weusi walikuwa na ujumbe kuwa maisha ya watu weusi pia ni muhimu nchini Marekani.

Mkanda wa video ulionesha maafisa wawili wa polisi walimwangusha mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 37 na kumpiga risasi mara kadhaa.

Hata hivyo, polisi wanajitetea kwa madai kuwa Bwana Sterling alipatikana akiwa amejihami kwa silaha.

Gavana wa jimbo la Luziana John Bel Edwards ametoa wito kwa utulivu wakati huu uchunguzi ukiendelea kuhusu tukio hilo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wamarekani weusi kuuawa katika mazingira kama haya.