MAREKANI-BARACK OBAMA-DALLAS

Barack Obama azuru Dallas katika mazingira magumu

Rais Barack Obama anatazamiwa kuwasili katika mji wa Dallas Jumanne hii Julai 12 kwa kutoa heshima kwa askari polisi watano waliouawa wiki iliyopita na kujaribu kuleta pamoja jamii iliyogawanyika kufuatia vurugu za polisi. Kazi ni kubwa, huku kukiwa na maandamano yanayondelea na watu wanaendelea kukamatwa.

Makao makuu ya polisi katika mji wa Dallas, Julai 10, 2016.
Makao makuu ya polisi katika mji wa Dallas, Julai 10, 2016. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu walikamatwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, wakati wa maandamano katika majimbo ya Louisiana na Mississippi, majimbo mawli kulikoshuhudiwa vurugu za polisi katika siku za hivi karibuni. Wamarekani wawili kutoka jamii ya watu weusi waliuawa na polisi katika matukio mbalimbali, wakati ambapo katika mji wa Dallas askari polisi ndio walilengwa.

Kwa upande wake Barack Obama amesema, hali sio nzui katika majimbo hayo. Rais Obama anakosolewa na yamii ya watu weusi kwa ukosefu wake wa uelewa dhahiri kwa waathirika wa utovu wa nidhamu wa polisi. Pia anakosolewa na vikosi vya usalama ambavyo vinabaini kwamba anaunga mkono maandamano ya kiraia. Usawa ni vigumu kuupata.

Matukio ya vurugu yanafuatana kwa miaka miwili sasa. Katika mji wa Charleston, wanadini weusi waliuawa na mfanyabisha meupe. Katika mji wa Orlando mashoga waliuawa kwa sababu za chuki na askari polisi waliuawa katika mji wa Dallas na mwanaharakati wa maandamano ya watu weusi wanaotia mbele machafuko.

Barack Obama amerejea kauli hii mara kadhaa akisema Wamarekani wanatakiwa kufanya kazi kwa kujichunguza na kuaminiana, lakini kipindi cha uongozi wake kiko mbioni kutamatika, na kazi bado ni kubwa.

Maafisa wa Zima Moto watoa rambirambi kwa wahanga wa mauaji yaliyosababisha vifo vya askari polisi 5 na kuwajeruhi wengine 9. Dallas, Julai 11, 2016.
Maafisa wa Zima Moto watoa rambirambi kwa wahanga wa mauaji yaliyosababisha vifo vya askari polisi 5 na kuwajeruhi wengine 9. Dallas, Julai 11, 2016. REUTERS/Carlo Allegri