MAREKANI-OBAMA-MAUAJI

Polisi wauawa Baton Rouge: Obama atoa wito kwa umoja

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa maeneo makali baada ya mauaji ya askari polisi watatu katika mji wa Baton Rouge, Louisiana, Julai 17, 2016 kutoka Ikulu ya Marekani.
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa maeneo makali baada ya mauaji ya askari polisi watatu katika mji wa Baton Rouge, Louisiana, Julai 17, 2016 kutoka Ikulu ya Marekani. REUTERS/Joshua Roberts

Mfululizo wa vitendo vya mauaji vinavyoendeshwa na Wamerekani weusi dhidi ya askari polisi wa Marekani vinaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya askari polisi watano kuuawa wiki iliyopita katika mji wa Dallas, askari polisi wengine watatu waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa Jumapili na mtu menye silaha katika mji wa Baton Rouge, ambapo kuliofanyika maandamano yenye vurugu kufuatia kifo cha Alton Sterling, Mmarekani mweusi, ambaye ni baba wa watoto watano, aliyepigwa risasi Julai 5 na maafisa walio amini kuwa anabebelea silaha.

Mtu aliyehusika na mauaji ya askari polisi Jumapili hii anatambuliwa kwa jina la Gavin Long, mwenye umri wa miaka 29, aliuawa kwa kupigwa risasi. Mkazi huyo wa jimbo la Missouri aliamua kuua askari polisi katika mji wa Baton Rouge katika kulipiza kisasi cha Alton Sterling? Polisi hawajui sababu ya mauaji hayo, yaliyoelezwa na Obama kama "kitendo cha ujinga".

"Kama taifa, ni lazima kuwa wazi: hakuna kinachohalalisha ukatili dhidi ya polisi. Mashambulizi dhidi ya polisi ni shambulio dhidi ya kila mmoja wetu. Ni heshima kwa sheria ambayo inafanya jamii kuwa jinsi ilivyo, " amesema rais wa Marekani Jumapili Julai 17.

Ubaguzi wa rangi

Hii ni mara ya 15 Rais Barack Obama akiwahutubia Wamarekani baada ya mauaji. Jumapili hii, alitoa wito kwa umoja wakati ambapo mvutano na ubaguzi wa rangi unaendelea kushuhudiwa na ambao umefikia kwa sasa kiwango cha kutisha wasiwasi: 63% ya Wamarekani katika utafiti uliofanywa na shirika la habari la Washington Post na kituo cha habari cha ABC News waliona kuwa uhusiano kati ya jamii umeshuka.

Wagombea urais katika uchaguzi wa urais nchini Marekani walitoa hisia tofauti. Kama Hillary Clinton amependekeza mwisho wa ubaguzi, Trump amelaumu uongozi mbaya na dhaifu na kuahidi kuwa rais wa sheria na utaratibu. Obama, kwa upande wake, amewataka Wamarekani kupunguza hasira kudhibiti kauli zao.